fbpx

Samsung Galaxy Fold: Simu ya kwanza ya display/kioo cha mkunjo kutoka Samsung

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Wengi walitegemea Samsung wangeonesha tuu simu hii na kusema itatoka mwishoni mwa mwaka au hata mwakani, ila Samsung wametambulisha na kusema itaanza kupatikana ndani ya miezi miwili kuanzia sasa – yaani Samsung Galaxy Fold itapatikana Aprili.

Samsung Galaxy Fold

Samsung Galaxy Fold: Kutoka Simu kwenda tabiti

Samsung wamekuwa na lengo la kuleta simu hii kwa muda sasa na miezi michache iliyopita Xiaomi walionesha ya kwao na hivyo ukawepo uwezekano wa wao (Xiaomi) kuwapiku Samsung kwa kuwa wa kwanza kuleta simu ya namna hii sokoni ila kumbe Samsung wapo mbele zaidi – simu ipo tayari kuingia sokoni.

Je, Samsung Galaxy Fold ni simu ya namna gani?

Kama jina lake lilivyo, ‘Fold’ ni kimombo cha kukunja/mkunjo, Galaxy Fold ndio jina waliloipa simu yao yenye uwezo wa kutumika kama simu na kisha pia kuweza kufunguliwa na kupata uso mpana zaidi na kuwa tabiti.

samsung galaxy fold

Muonekano ikiwa inatumika kama tabiti na ikiwa inatumika kama simu ya kawaida

Simu ya Galaxy Fold ikiwa imekunjwa ina kioo/display kidogo mbele ambacho unaweza kutumia kama simu ya kawaida wakati Galaxy Fold ikiwa katika umbo dogo – la inchi 4.6.

Pale utakapotaka kuitumia kama tabiti basi utaifungua na ndani ya sekunde moja programu tumishi yoyote uliyokuwa unaitumia wakati huo itajifungua kwa upana katika display/kioo cha ndani cha inchi 7.3 (sentimeta 18.5).

INAYOHUSIANA  Nubia Alpha: Simu janja inayovaliwa mkononi

Ukubwa huu unaifanya katika umbo la tabiti iwe na uwezo wa kufungua app tatu kwa wakati mmoja mbele ya mtumiaji kwenye display hii kubwa.

samsung galaxy fold

Samsung wamesema eneo la mkunjo wa simu hii linaweza kuhimili maelfu ya kuung/kufungua.

Kiungo chake kinachounganisha pande mbili Samsung wamesema wametumia teknolojia ya kisasa sana kuhakikisha kitadumu mara maelfu ya ufunguaji na ufungaji. Pande zote mbili zinahifadhi betri kuhakikisha kifaa hiki kinadumu na chaji muda mrefu – mAh 4380.

Galaxy Fold

Utumiaji wa programu tumishi tatu kwa wakati mmoja ndani ya Galaxy Fold

Galaxy Fold ina maeneo matatu yenye kamera – Nyuma kuna kamera tatu, ndani kwa ajili ya selfi kipindi unaitumia kama tabiti kuna kamera mbili, wakati unaitumia kama simu kuna kamera moja ya selfi.

INAYOHUSIANA  Sony Waja Na Toleo Jipya La Xperia, Xperia SL!

Sifa nyiingine; 

  • Inakuja na RAM ya GB 12,
  • prosesa ambayo Samsung hakuitaja – inaaminika itakuwa ni ya kwao na si Snapdragon.
  • Diski ujazo ni wa GB 512.
  • Inakuja na uwezo wa 4G na toleo la 5G lipo njiani.

Katika bidhaa ambazo Samsung wametambulisha hivi karibuni hii ndio bidhaa isiyo na uhakika sana wa hali ya soko. Ukiangalia bei yake ni kubwa sana na hili linaweza kuwafanya watu kuona ni rahisi zaidi kuwa na kununua tabiti na simu kama vitu tofauti.

INAYOHUSIANA  Tumia WhatsApp kwenye Kompyuta Yako Sasa

Toleo la 4G litaanza kupatikana mwezi wa 4 tarehe 26 kwa bei ya dola za Marekani 1,980 (zaidi ya Tsh. milioni 4.6).

Vipi una mtazamo gani na Samsung Galaxy Fold?

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.