fbpx
apps, Teknolojia, whatsapp

Mazungumzo kujifuta yenyewe kwenye WhatsApp

mazungumzo-kujifuta-yenyewe-kwenye-whatsapp
Sambaza

Kila siku teknolojia inakuwa na hii inatokana na mahitaji ya wadau kusababisha wataalamu kufikiria namna gani ya kuweza kutatua jambo fulani kwa wanufaa ya wadau/watumiaji. Kwenye WhatsApp huenda tukawa na uwezo wa kuamua mazungumzo kujifuta baada ya muda fulani kupita.

Utaonekana upo nyuma katika utandawazi iwapo hutumii simu ambayo ina WhatsApp au hata kukosa taarifa fulani kutoka kwa ndugu, jamaa/marafiki kwa sababu tu hutumii programu yenye watumiaji wengi zaidi duniani. Sasa hii ambayo wahusika wanaifanyia majaribio inaweza kuwafurahisha wengi na kuwachukiza wachache 😀 😀 😀 .

Sikii hii: Matoleo mawili ya majaribio (2.80.83 na 2.80.84) kuna kipengele kipya ndani ya mazungumzo ya faragha ambacho kinamuwezesha mhusika kuamua muda gani ujumbe/jumbe alizotuma zijifute mara tu saa, siku, n.k kutimia.

Mazungumzo kujifuta
Majaribio ya uwezo wa  mazungumzo kujifuta zenyewe bada ya muda fulani kwenye WhatsApp.

Sisi watumiaji wa WhatsApp tuna mambo mengi na si ajabu tukasahau kuwa tumebadilisha mpangilio kidogo sasa basi mara baada ya kuruhusu mabadiliko ujumbe utakotuma utaambatana na taarifa ya kukukumbusha baada ya muda fulani mazungumzo hayo yatafutika.

INAYOHUSIANA  Nguruwe kutumika kutibu upofu! #Sayansi #China
Mazungumzo kujifuta
Utakumbusha muda ambao mazungumzo yatajifuta iwapo utakuwa umeruhusu kipengele hicho.

Niishie tuu kwa kusema kuwa kipengele hicho bado kipo katika hatua za majaribio kwa whanaotumia matoleo hayo mawili niliyoyaanisha huko juu. Pengine maboresho hayo yakashangiliwa ama kuleta ugomvi kwa namna moja au nyingine 😛 😛 😛 .

Vyanzo: GSMArena, WABetaInfo

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|