fbpx
apps, Intaneti, Mtandao wa Kijamii, Teknolojia

Visa kwenda Marekani hadi utoe taarifa zako za mitandao ya kijamii

visa-kwenda-marekani-taarifa-mitandao-ya-kijamii
Sambaza

Sasa ni rasmi kwa wanaotaka Visa kwenda Marekani maombi yao yatahusisha kuorodhesha akaunti zao za mitandao ya kijamii.

Katika jambo la ajabu ni kwamba taarifa zitakazohitajika hazitakuwa za siku au muda huo bali watahitaji pia anuani za barua pepe na namba za simu ambazo umeshawahi kumiliki katika kipindi cha miaka mitano.

Kwa wenye uhitaji wa kufanya safari za kwenda Marekani kwa sasa itawabidi wajitathimini kwa undani na mambo wanayofanya au kusema kwenye mitandao ya kijamii. Ingawa Marekani ni taifa linaloheshimu sana uhuru wa maoni ila haitashangaza kama tweet au post moja ya mitandao ya kijamii uliyoongea dhidi ya Marekani kusababisha mtu mmoja anayehakiki data hizo kuamua kukunyima VISA.

INAYOHUSIANA  Google kupigwa faini ya kuvunja rekodi barani Ulaya
visa kwenda marekani
Visa kwenda Marekani: Inawezekana haitachukua muda mrefu tuone utaratibu huu kufuatwa na baadhi ya mataifa rafiki wa Marekani.

Historia: Visa ilianza kutumiza zaidi baada ya vitaa kuu vya kwanza vya dunia, ujio wa treni ulihakikisha watu wengi waliaanza kusafiri zaidi kati ya nchi moja hadi nyingine. Utoaji wa VISA huwa unafanyika kwa njia kadhaa: kuna njia ya kugongwa muhuri katika leseni ya kusafiria (passport), ugawaji wa karatasi au kitambulisho spesheli.

Je ni kwa kila aina ya mtu na kwa kila aina ya safari?

Ni watu walio kwenye kazi za kidoplomasia na baadhi ya watumishi wa serikali wanaosafiri kikazi ndio wataweza kunusurika na hitaji hili.

INAYOHUSIANA  Express WiFi: Huduma ya intaneti ya bei nafuu kutoka Facebook

Kwa nini sasa hivi?

Inaonekana Marekani wanachukua hatua nyingi zaidi za kuhakikisha wanachuja sana suala la watu kuingia nchini mwao. Utaratibu huu sio mpya ila zamani ulikuwa ni hitaji kwa watu wanaotoka kwenye mataifa yenye ugaidi tuu.

Je una mtazamo gani kuhusu utaratibu huu? Na kumbuka katika maelezo yao ni kwamba mtu yeyote atakayetoa taarifa za uongo au kuficha basi hiyo itakuwa ni sababu moja kuu ya mtu huyo kunyimwa VISA – ruhusa ya kuingia nchini Marekani.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |