fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Apple iCloud iCloud +

FAHAMU Kuhusu iCloud Plus!

FAHAMU Kuhusu iCloud Plus!

Spread the love

Katika mkutano mkubwa wa Apple unaofanyika kila mwaka unaojulikana kama Apple Worldwide Developers Conference (AWWDC) wa mwaka 2021 umegusia kuhusiana na iCloud plus (iCloud+).

Huduma hii inakua ya kimaboresho zaidi ukilinganisha na huduma ya iCloud ya kwanza ambayo tumeizoea. Ikumbukwe pia kuwa huduma ya iCloud ipo katika wigo mpana , kuanzia katika ujazo uhifadhi wa kimtandao, huduma ya barua pepe n.k

Huduma hii ya iCloud Plus inakua ni huduma ya kulipia kwa msimu na inakuja na vipengele vikuu vitatu ambavyo vinajulikana kama ‘Private Relay’, ‘Hide My Email’ na ‘Homekit Secure Video’.

iCloud Plus (iCloud+)

iCloud Plus (iCloud+)

Sasa Tuanze Kuchambua Kimoja Kimoja

Tuanze Na Hii Ya Kwanza ‘Private Realay’ 

Hii kazi yake kubwa sana itakua katika mtandao kwamba taarifa zinazoingia , kutumwa na kutoka zitakua haziwezi kufuatiliwa hata kidogo.

Hii inamaanisha hata Apple wenyewe wataakuwa hawana uwezo kabisa wa kuona taarifa hizo hata kama wakijaribu kuzifuatilia.

Hii imekaa kama ile ya end-to-end encryption sio?  utofauti wake ile ni baina ya mtu na mtu katika chati zao na hii ni katika mtandao kwa ujumla.

SOMA PIA  Apple kushitakiwa na kundi la watumiaji wa iPhone dhidi ya ukiritimba kwenye soko la Apps

Tuje Na Hii Ya Pili ‘Hide My Email’ 

Kipengele Cha Hide My Email

Kipengele Cha Hide My Email

Hichi ni kipengele ambacho kinapatikana katika Email, safari na maeneo mengine na kazi yake kubwa itakua ni kufika barua pepe yako.

Barua pepe hiyo itakua inafichwa kwa kuzalisha barua pepe nyingi nyingi ambazo ni feki na kuficha ile yako ambayo ni halisi hii inamaanisha kuwa faragha juu ya jambo hili itakua ya hali ya juu.

SOMA PIA  Apple Waja na Kava ya iPhone 6s Inayokupa Masaa 24 ya chaji

Tuje Na Ya Mwisho ‘Homekit Secore Video’ 

Hii ni teknolojia ya kamera za video ambazo zinakuwa nyumbani  na sehemu zingine kwa icloud ya mara ya kwanza ilikua ikiruhusu kamera tano lakini kwa iCloud Plus idadi haina mwisho.

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini sehemu ya comment, iCloud + imekaaje? je ni jambo zuri au ni jambo ambalo halina ulazima sana?

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Namba Moja Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania