fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Intaneti Tanzania TCRA Teknolojia

Safari ya Tanzania kuelekea teknolojia ya 5G

Safari ya Tanzania kuelekea teknolojia ya 5G

Spread the love

Nchi nyingi tuu duniani zimeshafikia kwenye kasi ya 5G ambayo inaeleza kuwa bora na ambayo itafanya matumizi ya intaneti kwenda kwa jinsi ukuaji wa teknolojia unavyokwenda.

Tanzania ina watumiaji wa intaneti zaidi ya milioni 25 mpaka hivi sasa wakiwa kwenye kasi ya 3G na 4G huku pia ikielezwa kuwa gharama za kununua vifurushi vya intaneti ipo chini kulinganisha na mataifa mengine.

SOMA PIA  Firefox Sasa Kupatikana Apple store Kwa Watumiaji wa iPad na iPhone

Waswahili husema “Kawia ufike” kauli hiyo ina maana ya kwamba ingawa inawezekana kabisa teknolojia ya 5G imechelewa kuja Tanzania lakini sasa safari inaanza ama kwa lugha rahisi wakati umefikia. Kupitia kwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabir Kuwe amebainisha kuwa yatafanyika majaribio ya teknolojia hiyo kwa lengo la kuongeza kasi ya huduma ya mawasiliano ya intaneti.

Safari

Uwezo wa 5G – Kasi ya 5G ikilinganishwa na teknolojia za nyuma.

Je, ni lini majaribio ya teknolojia ya 5G yatafanyika?

Ukweli ni kwamba haijawekwa wazi ni lini Tanzania itafanya majaribio ya teknolojia tajwa kwa lengo la kuongeza kasi ya intaneti na hatimae kuongeza ufanisi wa kazikwa watu mbalimbali ambao mawasiliano ya njia hiyo ni sehemu ya maisha lakini pia chanzo chamapato kwa mtu/watu bila kusahau serikali.

Inaelezwa kuwa sekta ya mawasiliano inasahika nafasi ya TANO katika kuchangia pato la taifa huku zaidi ya 25% ya watu wnwatumia simu janja.

TeknoKona inaamini safari ya ujio wa teknolojia ya 5G Tanzania utaongeza mambo mengi chanya hasa ukizingatia matumizi ya intaneti yana nafasi kubwa katika kuongeza ufanisi.

Vyanzo: Jamii Forums, AS News

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania