Ni mwaka mwingine ambapo nchini Tanzania yanafanyika yakiwa yameanza Mei 17-22 2021 yanayofanyika jijini Dar es Salaam pale jengo la LAPF Tower-Makumbusho, Kijitonyama kwa nyakati tofauti tofauti huku watu wakiweza kushiriki kwa njia ya mtandao pia.
Maadhimisho ya Wiki ya Ubunifu Tanzania yamekuwa yakifanyika kwa miaka saba saba sasa ambayo yamekuwa yakikutanisha wadau, serikali, sekta binafsi kuzungumza masuala mbalimbali yanayohusu Sayansi, Teknolojia na masuala mbalimbali ya kidijitali kwa ujumla wake.
Maadhimisho hayo ambayo yalitanguliwa na kilelele cha MASHINDANO YA KITAIFA YA SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UBUNIFU (MAKISATU) 2021 yaliyofanyika jijini Dodoma na kushudia vipaji mbalimbali kutoka kwa vijana wenye uwezo na akili ya kufanya vitu vizuri.
Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa alipokuwa akipatiwa maelezo na mmoja wa washiriki wa MAKISATU 2021.
Mara baada ya kumalizika kwa MAKISATU 2021 ikawa sasa ni zamu ya jiji la Dar es Salaam na mikoa mingine ambapo kwa mara ya kwanza maadhimisho hayo yanafanyika nje ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ambapo yatadumu kwa siku sita; kuanzia Mei 17-22 2021. Maadhimisho hayo yalizinduliwa jana na mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omary Juma Kipanga.
<aadhimisho hayo kwa mwaka huu yanabembwa na kauli mbiu UBUNIFU KWA UCHUMI WA KIDIJITALI STAHIMILIVU NA JUMUISHI ambapo wadau mbambalimbali wamekutana kujadili mada mbalimbali zikiwakutanisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania.
>Ukomo wa ufadhili kuko kwa MFUKO WA KUFADHILI UBUNIFU TANZANIA (HDIF). Kwenye siku ya kwanza ya maadhimisho hayo HDIF walibainisha kuwa hawatafadhili maadhimisho yajayo yaani mwakani na badala yake ulizinduliwa mradi mpya ulioitwa FUNGUO. Mradi huu ndio utakuwa unafadhili bunifu mbalimbali kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) na Umoja wa Ulaya ambazo pia zitakuwa zinaratibiwa na COSTECH.
>Maadhimisho kuanzia ngazi za chini. Wakati wa kufunga MAKISATU 2021 Mhe. Kassim Majaliwa aliagiza maadhimisho hayo sasa yaanzie wilaya kuja hadi ngazi ya taifa ili kutanua wigo wa upatikanaji wa wabunifu Tanzania.
>Maadhimisho kufanyika mikoa mbalimbali. Imeelezwa kuwa maadhimisho haya yatakwenda kwenye mikoa mbalimbali kamna vile Mwanza, Arusha, Tanga, iringa, Mbeya, Zanzibar, n.k. Kwa maelezo zaidi jinsi ya kushiriki/kujisajili kulingana na mkoa uliopo BOFYA HAPA.
Je, nani anaweza kushiriki?
Maadhimisho hayo kwa mkoa wowote ambao utapenda kushiriki ni BURE na pia mshiriki anaweza kuchagua kufika kwenye ukumbi ambao shughuli yenyewe inafanyika ama akashiriki kwa njia ya mtandao (kupitia Zoom, Google Meet).
Maadhimisho ya Wiki ya Ubunifu Tanzania kwa mwaka 2021 Dar es Salaam. Kauli mbiu ni “Ubunifu kwa Uchumi wa Kidjitali Stahimilivu na Jumuishi”.
Kazi kwao ewe mdau wa masuala ya teknolojia kwa njia yoyote kati ya mbili ambazo unaweza kushiriki kwenda kujifunza, kukutana na watu ambao mnaweza kushirikiana na kusogeza gurudumu la uchmu wa kidijitali lakini ambao ni jumuishi pia.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|
No Comment! Be the first one.