fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

tecno

Intaneti Teknolojia

Uwezo wa 5G upo vipi? Fahamu yote muhimu kuhusu teknolojia ya 5G

Uwezo wa 5G upo vipi? Fahamu yote muhimu kuhusu teknolojia ya 5G

tecno

Je unafahamu uwezo wa 5G? Sifa zake n.k? Makala hii itakusaidia kuweza kuelewa kwa undani teknolojia ya 5G. Hii ni moja ya teknolojia muhimu na kubwa katika sekta ya mawasiliano katika mwaka huu na miaka inayoendelea.

5G ni moja ya teknolojia muhimu kwa maendeleo ya sekta nyingi kwa sasa. Ni teknolojia ambayo hadi imesababishwa Marekani kuleta vikwazo vingi dhidi ya Huawei kwani hadi Marekani wametambua hii ni teknolojia itakayogusa karibia nyanja zote muhimu za uchumi na usalama.

Vifaa vya mawasiliano vya 5G – minara au ata simu, vinatumia umeme kidogo ukilinganisha na vile vya 4G. Kwa wastani wa zaidi ya mara nne.

Kasi ya 5G ipo vipi?

5G ni huduma yenye kasi ya kati ya mara 10 hadi mara 100 zaidi ukilinganisha na kasi unayoweza ipata kwenye teknolojia ya 5G. Mfumo mzuri wa 5G unaweza kufikia kasi za hadi Gigabits 10 kwa sekunde. Kwa matumizi ya kawaida ni kawaida kasi kucheza kati ya Mbs 150 hadi 500.

uwezo wa 5g

Uwezo wa 5G – Kasi ya 5G ikilinganishwa na teknolojia za nyuma

 

Katika mwaka 2020 ilitegemewa teknolojia itaanza kusambaa maeneo mengi zaidi, lakini kulikuwa na changamoto kadhaa zilizochelewesha mafanikio zaidi hii ikiwa ni pamoja na ujio wa janga la Covid19, vikwazo dhidi ya Huawei – ambao walikuwa tayari mbali zaidi katika teknolojia ya vifaa vya mawasiliano vya mfumo wa 5G.

GSMA – Chomo cha kimataifa kinachowakilisha makampuni/mashirika ya mawasiliana kimesema kwa mwaka 2020 Covid19 ilisababisha hasara ya asilimia 4-8 kwa makampuni ya mitandao ya simu.

GSMA wanaamini zaidi ya dola bilioni 890 zitatumika katika miaka 5 kuanzia sasa katika uwekezaji wa mifumo ya mitandao ya 5G duniani kote. Kufikia 2025 asilimia 20 ya intaneti ya simu itakuwa inatumika kupitia mifumo ya 5G.

matumizi ya 5g

Teknolojia ya 5G inagusa maeneo mengi zaidi ya kiuchumi kuliko teknolojia za nyuma. Katika ulimwengu ambao vitu vingi kwa sasa vinaunganishwa na huduma za intaneti teknolojia ya 5G itaongeza ufanisi wa vifaa vya aina mbalimbali

Hali ya kiteknolojia na nafasi ya Huawei

4G itaendelea kuwepo kwa muda mrefu. Mifumo mengi ya 5G iliyopo sokoni kwa sasa inabeba usafirishaji wa data/intaneti zaidi na huku 4G ikisimamia mawasiliano ya sauti na ujumbe mfupi. Mifumo inayoendesha yote hayo kwa 5G tayari ipo ila ni ya bei ya juu zaidi, tegemea baadhi ya mitandao kuanza na kuweka mifumo ya 5G kwa huduma intaneti tuu.

SOMA PIA  Microsoft na Facebook kujenga mkongo wa Intaneti ktk Bahari ya Atlantic

Huawei alianza kwa kasi zaidi katika utengenezaji wa vifaa vya mawasiliano ya 5G ila vikwazo vya Marekani vimewapa Siemens na Nokia nafasi nzuri ya kuwa mbele mwaka huu. Tayari Huawei wamepoteza mikataba ya kufunga mitambo ya mawasiliano ya 5G katika mataifa mengi Ulaya na nchi rafiki kwa Marekani. Huawei wanaweza fanikiwa kwenye baadhi ya nchi za bara la Asia pamoja na Afrika.

SOMA PIA  Twitter waleta QR Code, Kurahisisha kuwa-follow watu.

Ujio wa simu za 5G kwa wingi

Ingawa simu zenye uwezo wa 5G zilishaanza kupatikana katika miaka miwili nyuma kuanzia 2021 ndio tutaanza kuona uhamaji mkubwa wa simu na mitandao ya simu kwenda kwenye 5G. Simu ambazo zimekuja na teknolojia ya 5G kwa mwaka 2020 nyingi zilikuwa za bei ya juu, kwa mwaka 2021 ndio tutegemee kuona upatikanaji wa teknolojia hii ata kwenye simu za bei ya kati. Tutegemee kuona simu zinazokuja na uwezo wa 5G zinazocheza kwenye bei kati ya laki 5 hadi milioni 1.

Makampuni ya vipuri vya mawasiliano /chip kama vile Qualcomm kupitia chip za familia ya Snapdragon 600 na 400 wanategemea kufanikisha simu za bei ya kati kuweza kuja na teknolojia ya mawasiliano ya 5G kwa bei isiyo ya juu sana. Kampuni ya MediaTek nayo haipo nyuma, MediaTek ni watengenezaji maarufu wa chip za bei nafuu ukilinganisha na za Qualcomm.

Teknolojia ya 5G ni teknolojia itakayogusa karibia kila nyanja ya kiuchumi na maendeleo. Intaneti tayari ni moja ya teknolojia muhimu zaidi inayofanikisha biashara na ukuaji wa teknolojia nyingine nyingi.

Vyanzo: Thalesgroup, Android Authority, GSMA na vingine vingi
Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania