fbpx
Halotel, Intaneti, Kompyuta, Mitandao ya Simu, Tanzania, Teknolojia

NMB, Halotel kutoa huduma za TEHAMA bure mashuleni

huduma-za-tehama-mashuleni
Sambaza

Benki ya NMB na kampuni ya mawasiliano ya Halotel zimeingia mkataba wa makubaliano ya miaka miwili ya kutoa huduma za TEHAMA katika shule za serikali zaidi ya 200 hapa nchini.

Makubaliano hayo yamefanyika Agosti Mosi mbele ya waandishi wa habari na mwaka wa kwanza NMB itatoa kompyuta 350 kwa shule 100 na jukumu la Halotel litakuwa ni kuziunganisha na huduma ya intaneti.

Katika kuzipata shule hizo serikali itashirikiana na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Wizara ya Elimu.

huduma za TEHAMA
Mkurugenzi Mtendaji wa NMB Ineke Bussemaker (Kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Halotel Nguyen Van Son wakati wa makabidhiano ya mkataba wa kutoa huduma za TEHAMA mashuleni.

Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker amesema kwa kushirikiana na Halotel kila shule ambayo NMB itatoa kompyuta Halotel watatoa huduma ya intaneti na mahali ambapo Halotel watataka kupeleka Intaneti NMB itatoa kompyuta.

NMB ianataka kusaidia taifa na kuwa na watu wenye weledi hususani masuala ya TEHAMA bila kuwa na watu wengi wenye weledi hata biashara haziwezi kufanyika kwani mtu akiunganishwa na intaneti anakuwa ameunganishwa na dunia.

Upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Halotel, Nguyen Van Son amesema wao wako tayari kushirikiana na wadau wote wa maendeleo ya elimu nchini.

Hata hivyo, sio mara ya kwanza kwa NMB kutoa kompyuta katika shule kwani tayari imetoa kompyuta zaidi ya 600 katika shule mbalimbali na Halotel tayari wamekwishaunganisha intaneti zaidi ya kompyuta 417. Lakini hii ni kwa mara ya kwanza kwa kampuni hizo kushirikiana.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  YouTube GO - App ya YouTube isiyokula data sana
0 Comments
Share

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.