fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Android apps iOS

Apps 10 Zilizopakuliwa zaidi mwaka 2020! #Apps #Downloads #Android #iOS

Apps 10 Zilizopakuliwa zaidi mwaka 2020! #Apps #Downloads #Android #iOS

Je katika Apps 10 zilizopakuliwa zaidi mwaka 2020 unadhani app gani haiwezi kukosekana? App ya TikTok ndio app iliyopakuliwa zaidi kwenye simu janja kwa mwaka 2020. Kampuni ya Facebook pamoja na familia ya apps zake za WhatsApp, Facebook na Instagram bado zinaendelea kufanya vizuri pia.

app ya tiktok

TikTok bingwa.

Kwa mwaka 2020 app ya TikTok ilipakuliwa mara milioni 850 kwa watumiaji wa simu na tableti za iOS/Apple pamoja na zile za Android. Nyuma ya app hiyo ni familia nzima ya apps za kampuni ya Facebook, ambazo kwa pamoja zilipakuliwa mara bilioni 2.05.

SOMA PIA  'Soma Baadae': Huduma ya Kukuokoa ukiwa Mtandaoni

Apps za Facebook zashika namba 2 hadi 4.

App ya WhatsApp ilishika nafasi ya tatu ikiwa imeshusha mara milioni 600, huku app ya Facebook ikishika namba 3 kwa kushusha mara milioni 540, na nne Instagram ikishushwa mara milioni 503.

Mafanikio kutokana na janga la Corona – App ya mikutano ya Zoom namba 5.

Mwaka 2020 uliathiriwa na janga la Corona / Covid 19, janga hili lilisababisha vikao vingi vifanyike kwa mfumo wa mtandao. Katika eneo hili huduma ya mikutano ya kwa njia ya mtandao ya Zoom ilipata umaarufu sana na hii ikapelekea app yake kupakuliwa kwa zaidi ya mara milioni 477.

SOMA PIA  Tube Floating: Uwezo wa kuangalia video za YouTube wakati unatumia apps nyingine. #Android #Apps

Messenger, Snapchat, Telegram – nafasi ya 6, 7 na 8.

App ya kuchati ya Messenger (Facebook) ilishika nafasi ya 6 kwa kupakuliwa mara milioni 404, huku Snapchat ikishika nafasi ya 7 kwa kupakuliwa mara milioni 281 na huku app ya kuchati ya Telegram ikishika nafasi ya 8 kwa kupakuliwa mara 256.

App ya Telegram inaweza ikakua zaidi kwa mwaka huu kutokana na mabadiliko ya utumiaji data za watumiaji uliokuja kwenye app ya WhatsApp. Tayari Telegram inapakuliwa kwa kasi zaidi katika kipindi cha hizi siku chache kwa zaidi ya mara mbili kwa wastani wa kabla. Uamuzi huo wa Facebook umeshasababisha app zingine kama vile ya Signal na Telegram kuanza kupata umaarufu zaidi kutoka kwa watumiaji wanaopenda usalama wa data zao.

SOMA PIA  Samsung yazindua Samsung Galaxy J7 Prime 2 kitofauti na ilivyozoeleka

Namba 9 ni Google Meet, Namba 10 ni Netflix

App ya mikutano kwa njia ya mtandao kutoka Google, ya Google Meet ndio ilishika nafasi ya tisa na huku app ya Netflix ikifunga orodha hiyo.

apps zilizopakuliwa zaidi mwaka 2020

Apps zilizopakuliwa zaidi mwaka 2020

 

Chanzo: AppTopia

Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania