fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Intaneti Tanzania

Bei za GB Tanzania bado ni nafuu zaidi Afrika na ata Duniani. #Ripoti

Bei za GB Tanzania bado ni nafuu zaidi Afrika na ata Duniani. #Ripoti

Bei za GB a.k.a gharama ya kupata kifurushi cha GB 1 cha intaneti nchini Tanzania inabakia kuwa moja ya gharama nafuu zaidi Afrika na ata Duniani pia.

Katika ripoti ya kimataifa ya tafiti ya wastani wa gharama ya GB 1, World Mobile Data Pricing 2021, inaonesha kwa wastani Tanzania ipo kwenye kundi la mataifa yenye gharama nafuu zaidi ya data huku GB 1 ikiweza kupatikana kwa wastani wa Tsh 1,739.25, huku taifa la bei nafuu zaidi nchini Afrika likiwa ni Sudan – ambapo GB 1 inaweza gharimu takribani Tsh 630.

  • Kenya GB 1 ni takribani Tsh 5,217.75
  • Rwanda GB1 ni takribani Tsh 2,898.75
SOMA PIA  Clickfarms: Wauza Likes, Shares, na Comments wakamatwa nchini Thailand

Mabadiliko ya bei ya vifurushi iliyokuwa imefanyika miezi kadhaa nyuma kabla ya hatua za TCRA na serikali kufanyika yangepandisha sana gharama ya intaneti nchini na kutufanya tuwe kwenye kundi la bei ya juu.

Kupata uelewa mzuri angalia ramani hii kuelewa jinsi gharama za kupata GB 1 zilivyo katika mataifa mbalimbali. Rangi ya bluu iliyokolea inawakilisha bei ya chini ya Dola moja, kundi ambalo Tanzania ipo.

Uwekezaji mkubwa katika mkonge wa taifa wa intaneti pamoja na ushindani mkali kati ya makampuni ya simu Tanzania ni mambo ambayo yamechangia sana kuhakikisha gharama ya huduma hii muhimu kiuchumi na kijamii kwa sasa kuendelea kuwa ya bei nafuu.

Vyanzo: Cable
Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania