Watazania wengi tuu wameshatapeliwa mtandaoni na kusababisha fedheha kiasi kiasi cha kupeleka malalamiko yao polisi au kwenye mamlaka nyinginezo. Mwarobaini wa suala hilo umepatiwa njia rahisi ya kukabiliana nao kutoka TCRA.
Hakuna kitu ambacho kinaniuzi kwenye masuala ya mtandaoni kama kukutana na jumbe zinazoashiria harufu ya utapeli. Hii yote ni kutokana na utandawazi lakini pia tamaa ambazo mwisho wake huwa ni mbaya. Sasa wengi wetu tunaweza kufurahi kutokana na kwamba kuna mwarobaini kutoka TCRA ambao unalenga kuwasaka wahusika wa utapeli.
Nimefurahi sana kukutana na ujumbe muhimu kabisa kutoka kwa Mamla ka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambao unalenga kuwasaidia watanzania kuwasaka wale ambao wanatunga jumbe za udanganyifu. TCRA imetengeneza namba maalum, 15040 kwa ajili ya kupokea jumbe zenye zile namba za watu wanaotuma zile jumbe “……….ile hela uitume kweda namba hii……“.

Ni wazi kuwa jumbe za namna hiyo zina wakera watu wengi tuu na ifikie wakati sasa tusitumie ukuaji wa teknolojia katika upand e ambao si mzuri kwa kujinufaisha isivyo halali na sasa TCRA imerahisisha namna ambavyo watanzania wanaweza kuwaripoti wale wajanjajanja wa kubuni jumbe za kitapeli.
No Comment! Be the first one.