fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Mtandao Mtandao wa Kijamii whatsapp

Jinsi Ya Kujua Kama Ume’Blokiwa WhatsApp! #2021

Jinsi Ya Kujua Kama Ume’Blokiwa WhatsApp! #2021

Spread the love

Kwa watumaiaji wa mtandao wa WhatsApp kuna njia mbalimbali ambazo ziko kama viashiria kwamba mtu ameku’block katika mtandao wa huo.

Ni sawa viashiria hivi havina ushahidi wa asilimia mia kabisa kwamba ume’block’iwa lakini ni moja ya namna ya kujua- sijui kama naeleweka!

WhatsApp

WhatsApp

Kumbuka mtandao wa WhatsApp haukutaarifu moja kwa moja kama ume’block’iwa hivyo basi inakubidi tuu kutumia njia mbadala ili kujua hivyo.

Viashiria Hivyo Ni Kama Ifuatavyo!

  • Angalia Last Seen au Online Status
SOMA PIA  YouTube yafanya mabadiliko ya logo!

Kama unahisi mtu amekublock kwa haraka haraka angalia kama unaweza kuona status zake (kama anapost) na pia angalia ‘last seen’ yake. lakini hapa kumbuka kama atakua amezima (kuamuru kutoonesha) kupitia settings basi hutaweza kuona.

  • Angalia Katika Profile

Kaa ukijua kama mtu amekublock katika mtandao wa WhatsApp kamwe huwezi kuona picha yake katika profile. Hutoweza kuona hata kama akibadilisha tena picha.

  • Jaribu Kumtumia Meseji

Hapa hata ukituma meseji kama mtu ameku’block basi kaa ukijua kwake itamfikia meseji ambayo imepiga tiki moja tuu. Hii ni tofauti maana kwa mtu ambae hajaku’block kwa kawaida meseji zinaanza kupiga tiki moja alafu zinafuata kuwa mbili.

  • Jaribu Kumpigia Simu (Kwa Kutumia App Ya WhatsApp)
SOMA PIA  Angalia Nani 'Analipotezea' Ombi Lako La Urafiki Facebook!

Kama amekulamba block kaa ukijua hata ukijaribu kumpigia simu basi simu hiyo haitatoka (haitomfikia). Utaona tuu ujumbe unaosema  ‘Calling’ lakini hutoona simu hiyo ikiandika ‘Ringing’ au ikipokelewa.

  • Jiunge Group Moja Na Unaehisi Ameku’Block

Kama utaunga group lako na mtu ambae unahisi ameku’block, ukisha maliza utashangaa ndani ya ‘group’ uko mwenyewe.

ujumbe kutoweka whatsapp

Uso Wa Kutuma Ujumbe Katika WhatsApp

Hivyo ni baadhi ya viashiria vinavyoonyesha kuwa mtu amekublock katika mtandao wa WhatsApp. Kama unahisi kuna mtu amekublock basi fuatulia mbinu katika vipengele vyote ili kuwa na uhakika zaidi.

SOMA PIA  "Unaweza Nisikia ....?" - Snowden Ajiunga Twitter

Ningependa kusikia Kutoka Kwako, Niandikie Hapo Chini Katika Eneo La Comment, Hii Umeipokeaje? Vile vile Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Maana Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania