fbpx

Honor Magic 2 mbele ya macho yetu

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Simu za Honor zipo toleo tofauti tofauti ambazo tayari zipo sokoni na kuendelea kuleta ushindani. Hata hivyo, Honor Magic 2 ilizinduliwa bila ya wengi kutegemea.

Wakati wa tamasha la IFA lililofanyika jiji la Berlin-Ujerumani Afisa Mkuu Mtendaji wa Huawei alikuwa akizindua Huawei Play lakini ghafla akawashangaza watu kwa kutoa Honor Magic 2 mfukoni mwake. Sifa za simu hiyo ni kama ifuatavyo:-

Kipengele

Honor Magic 2

Kioo Kioo kina urefu wa inchi 6.39  huku teknolojia ya kwenye kioo ni AMOLED
Muonekamo Ina vitu ambavyo vimejificha hivyo basi inahitajika kuwa mjanja kidogo kuweza kuviona
Kipuri mama HiSilicon Kirin 980 ndio iliyowekwa kwenye simu husika
Honor Magic 2

Honor Magic 2 haina umbo la herufi “V”.

Kipengele

Honor Magic 2

Kamera Nyuma: Kamera tatu-mbili zina MP 16 na ile kuu ina MP 24.

Mbele: Ina kamera tatu; moja ina MP 16 na mbili zina MP 2 kila moja

Itakubidi ubonyeze kidogo kwa kwenda chini ili kuweza kuziona/kutumia kamera za mbele.

RAM/Diski uhifadhi
  • 6GB RAM kwa 128GB memori ya ndani na
  • 8 GB RAM kwa 128/256GB memori ya ndani
Betri
  • 3500 mAh ndio nguvu ya betri na haliwezi kutoka,
  • Pia ikiwa na teknolojia ya kuchaji haraka; nguvu ya 40W,
  • Haina teknolojia ya kuchaji bila waya.
Honor Magic 2

Kamera za mbele mara baada ya kubofya na kushusha chini kidogo uso wa mbele.

Kipengele

Honor Magic 2

Bei

$489|Tsh. 1,124,700 (6/128GB), $589|Tsh. 1,354,700 (8/128GB) na $689|Tsh. 1,584,700 (8/256GB)

Rangi

Nyeusi, Bluu mpauko na Zambarau

Mengineyo

  • Inatumia kadi mbili za simu kiwango cha GSM / CDMA / HSPA / LTE,
  • Imewekwa Android 9 Pie,
  • Haina redio wala sehemu ya kuchoka spika za masikioni,
  • Ulinzi wa kutumia alama ya kidole upo ndani ya kioo,
  • Inatumia OTG USB, teknolojia ya FaceID nayo ipo.
INAYOHUSIANA  Dondoo kuhusu Samsung Galaxy Note 10 Pro

Hiyo ndio Honor Magic 2 ambayo ilitangazwa mwezi Oktoba 2018 ambayo inaongeza idadi ya simu kutoka za familia husika (Honor).

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.