fbpx

Google Playstore ina muonekano mpya

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Soko maarufu kwa ajili ya kuweza kupakua programu tumishi zilizohakikiwa na rasmi zipo kwenye “Google Playstore” kwa simu yoyote ambayo inatumia mfumo endeshi wa Android.

Katika siku za karibuni Google wameboresha muonekano wa soko lao mahususi kwa programu tumishi mbalimbali ambazo zimetengenezwa kufanya kazi kwenye vifaa vya Android.

Vitu ambavyo vimeboreshwa vinahusisha kuweka vitu katika mpangilio wa makundi ili iwe rahisi kwa mtumiaji kuweza kupata kile anachokihitaji kwa urahisi zadi (bila kusumbuka).

muonekano mpya

Playstore: Muonekano mpya (kushoto)|Muonakano wa zamani (kulia).

Lakini pia kwenye huo muonekano mpya utaona maboresho upande wa rangi kwa kuondoa rangi ya kijani iliyodumu kwa miaka mingi na badala yake hivi sasa ipo rangi nyeupe hasa kwenye kipengele cha mpangilio.

muonekano mpya

Eneo jingine lililonakshiwa katika muonekano mpya wa Google Playstore.

Toleo hilo jipya ni la nambari 12.6.13 na ili kulipata utatakiwa kupakuwa masasisho yake au au utumie njia ya kushusha Google Playstore APK la toleo jipya kabisa.

Vyanzo: GSMArena, The Android Soul

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Matangazo kwenye WhatsApp Status yapo njiani kuja 2020
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.