Sokoni kuna simu janja nyingi tuu ambazo zinashindana kwa sifa zao kuvutia wateja na hatime kuuzika. Huawei wameendelea kutoa rununu toka nitoke na sasa tunazungumzia Huawei nova 8i.
Kwa miaka kadhaa nimekuwa nikifuatilia simu janja za Huawei mbalimbali zikiwemo toleo la “Nova” ambazo hadi sasa zimefikia tano ( nova 8 5G, nova 8 Pro 4G, nova 8 Pro 5G, nova 8 SE na nova 8i) na kama kawaida yangu jicho langu likakutana na Huawei nova 8i nikasema nilete sifa zake kwako ewe msomaji wetu.
Ubora wa kioo|Kipuri mama
Mimi ni mpenzi wa simu janja ambazo kioo ni kipana na si haba makampuni mengi wanatoa rununu ambazo ni pana. Simu hii ina kioo chenye urefu wa inchi 6.67, ung’avu wa hali ya juu, haina kingo pembezoni. Kwenye upande wa kipuri mama hapa ni Snapdragon 662 SoC.
Uwezo wa betri|Kamera
Uwezo wa betri halikadhalika teknolojia ya kuchaji haraka, ubora wa kamera vimekuwa moja ya vitu ambavyo naviangalia kwa jicho la karibu wakati wa kufanya maamuzi ya simu janja gani ninunue. Kwenye simu hii Huawei wameiwezesha na 4300mAh, 66W upande wa kuchaji haraka (60% kwa dakika 17, 100% ndani ya dakika 38).

Diski uhifadhi|Mengineyo
Kipengele cha memori kwenye simu janja huwa kina mvuto wa kipekee hasa katika ulimwengu huu wa kisasa zaidi. Simu hii inapatikana katika toleo mbili tofauti kwa maana ya kwamba RAM ni GB 6 au 8, diski uhifadhi-GB 128. Inakuja na Android 10. Rangi za simu hii ni Nyeusi, Bluu na Fedha.

No Comment! Be the first one.