fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Intaneti Tanzania TCRA Teknolojia

Fahamu kuhusu kanuni ndogo mpya zinazosimamia mitandao ya simu. #TCRA

Fahamu kuhusu kanuni ndogo mpya zinazosimamia mitandao ya simu. #TCRA

Mwezi Februari umeisha kwa maumivu makubwa kwa watumiaji wa intaneti baada ya kuona mitandao ya mawasiliano ya simu ikipandisha gharama za intaneti kwa asilimia kubwa bila sababu za msingi kutolewa.

Kumbuka kwa muda mrefu tayari kulikuwa pia na malalamiko ya wateja juu ya upoteaji wa data unaotia shaka ya kwamba kuna baadhi ya mitandao ya simu inafanya mahesabu vibaya kwenye utumiaji wa vifurushi vya data. Leo TCRA wametambulisha rasmi kanuni ndogo walizokuja nazo ili kutatua baadhi ya changamoto za muda mrefu zinazohusisha huduma za mitandao ya simu hasa kwenye gharama za huduma za mawasiliano (dakika na data).

intaneti faini milioni 5 laini Fahamu kuhusu kanuni ndogo mpya

Hili ni jambo jema ingawa bado changamoto ya ubadilishaji wa ghafla wa bei za vifurushi haujaelezewa.

Baadhi ya mambo yaliyomo katika Kanuni ndogo hizo ni pamoja na:- 

1. Mtoa huduma hatatoa huduma za vifurushi bila kibali cha Mamlaka; 

2. Mtoa huduma atahakikisha kwamba bei za vifurushi zinazingatia bei husika ya chini na ya juu zilizowekwa na Mamlaka; 

3. Mtoa huduma atatumia lugha rahisi na vigezo na masharti yaliyo wazi kuhusu vifurushi vinavyotolewa; 

4. Vifurushi vinavyotolewa kwa Mtumiaji havitaondolewa, havitarekebishwa au kubadilishwa ndani ya miezi mitatu baada ya kuidhinishwa; 

5. Mtoa huduma atatoa fursa kwa Mtumiaji wa huduma za mawasiliano kuchagua na kujiunga na vifurushi visivyokuwa na ukomo wa muda wa matumizi vitakavyo patikana kwenye menyu kuu na watatumia jina linalofanana kwa vifurushi hivi ili vitambulike kwa wepesi; 

6. Mtoa huduma atatoa taarifa kila wakati matumizi ya kifurushi yatakapofikia asilimia 75 na 100 kwa vifurushi vya muda wa maongezi, data na SMS; 

7. Mtoa huduma ataweka Program Rununu (Mobile App) ya kumwezesha mtumiaji wa huduma mwenye simu janja kufuatilia matumizi yake ya data kwa kupakua Program Rununu hiyo ya mtoa huduma; 

8. Mtoa huduma ataweka utaratibu unaowawezesha anayejiunga na huduma za vifurushi kuchagua na kukubali kutozwa gharama zisizokuwa kwenye vifurushi mara muda wa vifurushi alichojiunga nacho au uniti za kifurushi husika kumalizika. 

Utaratibu huu wa kuchagua na kukubali utakuwa chaguo msingi mpaka pale anayejiunga achague na kukubali kutumia gharama nje ya kifurushi; 

9. Mtoa huduma ataweka utaratibu wa kumwezesha aliyejiunga na kifurushi chochote kuendelea kutumia muda au uniti za kifurushi ambazo zitakuwa zimesalia ndani ya muda wa matumizi uliowekwa kwa kununua tena kifurushi hicho hicho kabla ya kumalizika kwa muda wake; 

10. Mtoa huduma ataweka utaratibu au mfumo wa kumwezesha mtumiaji wa huduma kuhamisha uniti za kifurushi kwenda kwa mtumiaji mwingine ndani ya mtandao wake kwa masharti kwamba: 

Kiasi cha chini cha kuhamisha kitakuwa ni 250Mb na Mtumiaji anaweza kuwahamishia watumiaji wasiozidi wawili; na 

Mtumiaji aliyehamishiwa Uniti za Kifurushi hataruhusiwa kumhamishia Mtumiaji mwingine uniti hizo au sehemu ya uniti alizohamishiwa; 

SOMA PIA  Samsung kuzindua memori kadi ya 512GB

11. Mtoa huduma hataruhusiwa kupunguza kasi ya data kwenye kifurushi cha Mteja ndani ya muda wa kifurushi husika; 

12. Mtoa huduma hatafanya Promosheni zaidi ya tatu au kutoa ofa maalum zaidi ya tatu kwa wakati mmoja kupitia huduma za sauti, SMS na data; 

Utekelezaji wa Kanuni ndogo hizi utaanza rasmi tarehe 02 Aprili, 2021 na tunaamini utaendelea kujibu mambo mengi yanayolalamikiwa na wateja kwa sasa. 

Je, una mtazamo gani juu ya sheria hizi ndogo?

Chanzo: TCRA

SOMA PIA  Facebook Wampa Mtoto wa Miaka 12 Dola $10,000 kwa ku'hack Instagram
Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Comments

  1. Robinson mworia - March 2, 2021 at 21:43 - Reply

    Ni vizuri kwa marekebisho haya yakazingatia pia kuwa mteja hapaswi kupangiwa muda wa kutumia yani ukomo!
    Kwa mfano eti mteja unajiunga alafu unapangiwa lazima utumie ndani ya 24 hrs huu ni uhuni

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania