fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Apple iOS 14 simu Teknolojia

iOS 14 imewafikia watumiaji kwa asilimia ngapi mpaka sasa?

iOS 14 imewafikia watumiaji kwa asilimia ngapi mpaka sasa?

Kutumia toleo la karibuni kabisa linalohusisha programu endeshi au masasisho mengine yanayotolewa kwa maana ya kukifanya kifaa kiwe salama zaidi si jambo la kupuuzia hata kidogo na hii ni wa watumiaji wa Android halikadhalika iOS.

Ni miaka karibu miaka kumi na minne sasa tangu iPhone ya kwanza itoke huku ikiwa na mfumo endeshi wa iOS 1 na sasa imefikia toleo la 14 na kuzidi kupata wateja wengi zaidi kila baada ya kipindi fulani. Unafahamu sifa za iOS 14? Soma zaidi kwa KUBOFYA HAPA.

SOMA PIA  Ipate Simu Yako ya Android Kupitia Google Search

Kwa watumiaji wa iPhone kuanzia toleo la 6s mpaka iPhone SE 2020 wanaweza kushusha toleo hilo, iPhone 12 na familia yake nzima zenyewe zinakuja zikiwa na iOS 14 tayari.

Kwa mujibu wa takwimu za karibu kabisa kutoka kwa Mixpanel zinaonyesha kuwa mpaka sasa 90.45% wanatumia iOS 14. Mwezi Februari, Apple ilisema iOS 14 ilishafika 86% kwa vifaa vyote vilivyotoka ndani ya miaka minne iliyopita, 80% ya iPhone zinatumia iOS 14.

watumiaji

Takwimu za Mixpanel zikionyesha ni kwa kisi gani iOS 14 imewafikia watumiaji wake.

Kwa haraka haraka tuu takwimu  za karibu zinaonyesha ni 11% pekee ndio wanatumia Android 11 nchini Marekani? Je, wewe iPhone yako inatumia toleo la karibuni kabisa? Namaanisha iOS 14.5.

TeknoKona tumekuhabarisha hivyo basi usiache kutufuatilia kila inapoitwa leo.

Vyanzo: 9to5Mac, GSMArena

SOMA PIA  TB 2 - USB Flash Drive yenye ujazo mkubwa zaidi yatambulishwa!
Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania