fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Android LG simu Teknolojia

LG kuendelea kutoa masasisho ya Android kwa baadhi ya simu zake

LG kuendelea kutoa masasisho ya Android kwa baadhi ya simu zake

Duniani kote wanafahamu kuwa LG inajiandaa kufungasha virago kwenye biashara inayohusisha simu janja lakini jambo hilo si la kufurahisha hasa kwa wale ambao wanazipenda rununu za kampuni hiyo. Umuhimu wa masasisho ya Android ndio inawasukuma LG kuendeleza huduma hiyo ingawa itakuwa ni kwa baadhi ya simu janja.

Taarifa zinasema katika kipindi kinachokaribia miaka sita LG wamepata hasara ya jumla $4.5 bilioni na mwisho wa mwezi Julai LG watasema “Kwaheri” kwenye bishara ya simu janja mara baada ya kudumu kwenye soko la ushindani wa simu janja kwa zaidi ya miaka saba.

SOMA PIA  Ushauri wa Simu ya kununua kulingana na Bei / Bajeti

Hata hivyo, uamuzi huo una maumivu lakini unakuja na faraja ndani yake kwani kwa baadhi ya wateja wenye simu janja walizonunua kutoka kwenye kundi la “Premium” wataendelea kupokea masasisho ya Android mara tatu katika vipindi tofauti mara baada ya kuacha biashara ya simu janja na rununu zitakazohusika ni zile zilizotoka 2019 na kuendelea ndio zipo kwenye mpango huo.

Unazijua simu janja za LG zilizotoka 2019 na kuendelea?

Watu wote duniani kote wenye LG kutoka familia ya “G” za 2019 kuendelea, LG “V” kama Velvet, LG Stylo na LG zenye mtiririko wa “K” ndio zitaendelea kupokea masasisho yanayohusu programu endeshi katika kipindi cha miaka mitatu lakini bila kusahau kuwa ni zile ambazo zipo kwenye kundi la “Premium” tu ndio zimejumuishwa kwenyempango huo.

masasisho ya Android

Simu ya LG Wing ambayo pia ipo kwe orodha ya zile rununu ambazo zitaendelea kupokea masasisho ya Android mara baada ya wahusika kufunga biashara.

LG ndio hao wameona kuwa inatosha sasa kibarua kinabaki kwetu na hasa kujipanga na kuweza kufahamu namna ya kusonga mbele kwani kupakuwa masasisho kitu kitu cha muhimu sana kwa usalma wa vifaa vytu vya kiganjani.

Vyanzo: Gadgets 360, Android Authority

SOMA PIA  Kupanda kodi kwa baadhi ya makampuni
Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania