fbpx

Android, iOS 14, Maujanja, Teknolojia

Je, unataka simu yako ya Android iwe na muonekano wa iOS 14?

je-unataka-simu-yako-ya-android-iwe-na-muonekano-wa-ios-14

Sambaza

Wakati fulani rafiki yangu alinishangaza pale niliposhika simu yake ya Android na kuona muonekano wa uso wa mbele pamoja na mpangilio wa programu tumishi kama kwenye toleo la iOS 12 nikavutiwa kutaka kujua mbinu hiyo na ndipo aliponifunuga macho kumbe hata wanaotumia Android unaweza ukasema “Wamehamia” kwenye iPhone.

Dunia inafahamu kuwa iOS 14 imeshatoka na wenye iPhone (kuanzia iPhone 6s na kuendelea) wanafurahi kutokana na vile ambavyo vipo kwenye programu endeshi husika. Sasa wanaotumia Android na wao wanaweza kupata angalau kionjo cha iOS 14. Swali ni je, kivipi?

Kwa yeyote ambaye anatumia simu inayotumia Android basi itambidi kupakuwa programu tumishi iitwayo KWGT kutoka kwenye Playstore lakini piaΒ KWGT Pro nje ya soko la programu tumishi (unapakuwa ya toleo la APK) kisha unafuata hatua zote za kuweza kuiweka kwenye simu yako ya Android.

Mara baada ya kushusha KWGT Pro ndani yake utakuta kuna programu ndogondogo ambazo ukizitunza kwenye simu uso wa mbele utabadilika kulingana na kile ambacho umekihifadhi hivyo kubadilisha mambo yalivyokuwa hapo awali.

simu yako ya Android
Kumbuka kubofya “Save once” mara baada ya kuchagua kile unachotaka kukihifadhi kwenye simu yako ya Android.

kwenye KWGT Pro utaweza kupata aina mbalimbali za muonekano hivyo kubadilisha kabisa muonekano/mpangilio wa programu tumishi bila kusahau unaweza kufanya rununu ikaonekana kama unatumia iOS 14 πŸ˜† πŸ˜† πŸ˜† .

simu yako ya Android
Unaweza kubadilisha kabisa sura ya simu yako ya Android kwa kutumia programu tumishi-KWGT.

Kutokana na sababu mbalimbali unaweza ukawa huna uwezo wa kumiliki iPhone inayokubali toleo la iOS 14 lakini hiyo isiwe shida kwani kwa kutumia programu tumishi fulani na wewe unaweza kuifanya rununu ionekane ya kitofauti sana.

Chanzo: Android Central

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: , ,

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*