WhatsApp wameleta huduma yao ya WhatsApp Web kwa Firefox na Opera, baada ya kuanza kuitangaza mara ya kwanza kwenye Google Chrome.
Tayari tumezungumzia njia moja fupi ya Kufungua WhatsApp kwenye Firefox na sasa tumepata njia fupi na labda ya rahisi zaidi ukiwa unatumia kivinjari hicho. Njia hii ni kupitia kisaidizi cha WhatsApp Panel cha msanifu wa programu aitwaye Alejandro Brizuela.
Kisaidizi cha WhatsApp Panel kinaianzisha Whatsapp na kuiweka kwenye eneo linaonekana kirahisi unapokuwa unatumia Firefox.
Kisaidizi hiki kinafanya kazi za msingi za mawasiliano ya WhatsApp ila tu ina kasoro kadhaa amabazo hata hivyo haziharibu mazungumzo ya kawaida kama:-
>Hautaweza kutumia sauti
>Hautafungua menu kwa kliki ya kushoto
>Hautaweza kuchukua picha kwaa web-cam
Pakua kisaidizi hiki na anza kuitumia WhatsApp vyema kwenye Firefox hapa
Kutumia WhatsApp kwenye Kivinjari chako soma:
Picha Na: Dotekomanie, Giga.de
No Comment! Be the first one.