Hivi ushawahi kufikiria kama siku hizi kuna App ya kila kitu? Maana zimekua nyingi sana na ukiachana na yote kuna zinazokula ujazo wa simu na zingine zinakula betri na vyote kwa pamoja!.
Katika tafiti fupi iliyofanyika na pCloud unaonyesha kuwa asilimia 93 ya watumiaji wa simu janja wanatumia App ambazo zinafanana na kwa kiasi kikubwa App hizi ni kwamba zinakula sana chaji au kujaza nafasi katika simu janja
Kuna mambo mengi ya kuzingatia ili kujua ni App gani zinakula chaji mfano kuna App zingine ili kufanya kazi zinaitaji vitu vingine kugunguka kama vile ‘Location’, WiFi, ‘Microphone’ na kamera (mfano mzuri WhatsApp)
Kutokana na utafiti huo ni wazi kwamba mitandao ya kijamii ndio inaongoza kwa wingi kwa kumaliza chaji za simu (kuua betri la simu)
App zingine ni kinara zaidi katika swala zima la kuchukua nafasi nyingi katika simu, list nzima ni kama invyoonekana hapa chini (kwenye picha)
Tafiti hii wakati inafanyika vipengele vilivivyozingatiwa ni App yenyewe wakati inafanya kazi inatumia vitu gani vingine vya ziada. Kwa mfano kuna baadhi ya App zinatumia teknolojia ya dark mode ambayo huwa inaifanya App kutumia chaji kidogo kuliko zile ambazo hazina teknolojia.
No Comment! Be the first one.