fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
simu

Tazama Mabadiliko ya Kimuonekano Matoleo ya Samsung Galaxy S

Tazama Mabadiliko ya Kimuonekano Matoleo ya Samsung Galaxy S

Spread the love

Samsung wanatengeneza na kuingiza sokoni simu za aina mbalimbali kila mwaka, ila ni matoleo machache yanapata kupewa nafasi ya kipekee kabisa hii ikiwa ni pamoja na bajeti kubwa ya kuzitangaza.

Familia ya simu zake zinauzika zaidi na hivyo kupewa nafasi ya kipekee kabisa katika kampuni hiyo ni matoleo ya simu za Galaxy S. 

samsung_i9000_galaxy_s-17 (3)

Hii ndio simu ya kwanza iliyokuja na jina la Galaxy S, baada ya mafanikio makubwa kimauzo ndio toleo lililofata likaitwa Galaxy SII

Toleo la kwanza, yaani Samsung Galaxy S liliingia sokoni mwezi wa 6 mwaka 2010, na kwa kipindi hicho ndio ilikuwa simu nyembamba zaidi sokoni, toleo hili hadi kufikia mwaka 2013 limeshauzika kwa idadi ya simu milioni 25.

SOMA PIA – Hizi Ndizo Simu 20 Zilizouzika Zaidi Duniani Hadi Sasa!

Mtandao wa GadgetLove umezikusanya picha za tokea toleo hilo la kwanza kabisa na matoleo yote yaliyofuata baada ya hapo. Hii inakusaidia kuona mabadiliko mbalimbali ya kimuonekano yaliyotokea katika matoleo hayo hadi kufikia hili la juzi la Samsung Galaxy S6. Tazama mabadiliko hayo kwenye video hii fupi. SOMA PIA – Fahamu Samsung Galaxy S6 na S6 Edge

SOMA PIA  Wezesha Intaneti Kwenye Simu/Tableti ya Android!

Kwa picha ya kawaida, kama GIF hapo juu imesumbua kuonekana basi utofauti wake kwa haraka ni kama hivi;

History-of-the-Samsung-Galaxy-S-Series-Infographic-770x350

Je ubunifu upi wewe umeupenda zaidi?

Tungependa kusikia kutoka kwako. Tuandikie mawazo yako sehemu ya maongezi kwa chini na pia kumbuka kusambaza makala hii kwa ndugu na marafiki.

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania