fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Infinix simu Smartphones

Simu Ya Kwanza Ya Android Kuja Na Processor Ya ‘CHIPSET HELIO G96’ Yatua Rasmi Bongo!

Simu Ya Kwanza Ya Android Kuja Na Processor Ya ‘CHIPSET HELIO G96’ Yatua Rasmi Bongo!
Spread the love

Week moja nyuma kampuni ya simu Infinix ilizindua rasmi simu ya kwanza ya Android kuja na Gaming processor yenye uwezo mkubwa….

….zaidi ‘MediaTek Helio G96’ ambayo ni Infinix NOTE 11 pro pamoja na Infinix NOTE 11 yenye teknolojia ya AMOLED kwa upande wa kioo.

Rangi Mbali Mbali Za Infinix Note 11 Pro

Rangi Mbali Mbali Za Infinix Note 11 Pro

Infinix NOTE 11 na NOTE 11 pro ni simu bora kwa mazingira yetu ya kazi kutokana na uwezo wa processor na kioo kuzifanya simu hizi kuweza kufanya vitu vingi kwa haraka zaidi katika muda mfupi na pasipo kuwa na matumizi makubwa ya chaji.

Kamera Ya Infinix Note 11

Kamera Ya Infinix Note 11

Processor ina faida kubwa sana hiki ni kipengele muhimu kwenye simu kwa mtu ambaye anaifahamu simu vizuri basi kipengele cha kwanza kuzingatia ni processor

SOMA PIA  Kodi kwa Facebook, Google kuwa juu

Processor ndio inafanya programu zote za simu kufanya kazi kwa haraka na wepesi lakini pia inasaidia simu iweze kuishi na chaji kwa muda mrefu sababu spidi kubwa ya processor inapunguza unyonywaji wa chaji.

Infinix Note 11 Pro..

Infinix Note 11 Pro..

Kioo cha AMOLED kina sifa nyingi na hii ni kutokana kioo hiki kina layers chache hadi kuifikia simu yenyewe ndani hivyo basi AMOLED inakupa faida hizi simu kudumu zaidi na chaji, picha zenye rangi asilia lakini pia tunasema inarespond kwa haraka wakati wa kuperuzi.

SOMA PIA  Fununu kuhusu Google Pixel 4a

Kwa mujibu wa Infinix hizi simu mbili zinalenga zaidi kurahisisha kazi ambazo zingewezwa fanywa na computer au kamera ya digitali basi kufanyika na NOTE 11 series ili kuokoa muda na kuleta wepesi zaidi wa kazi.

Muonekano Wa Kamera Ya Infinix Note 11

Muonekano Wa Kamera Ya Infinix Note 11

Sifa nyingine za simu hii ya Infinix NOTE 11 pro ni teknolojia ya ‘refresh rate’ ambayo inanyuzi  120 ambayo inaifanya Infinix NOTE 11 pro kutopoteza ubora wake wa kuchakata kazi kwa haraka.

SOMA PIA  SAMSUNG Kutengeneza Simu ya Kukunja (flip phone) Tena

Simu hii vile vile ina kamera tatu nyuma na kamera kuu ni Megapixel 64 na zoom lens 30x inayofanyika na moja kati ya camera za nyuma yenye Megapixel 13.

Infinix NOTE 11 series zimeanza kupatikana rasmi katika maduka yote ya simu inchini Tanzania zikiwa na ofa ya GB96.

Kujua Zaidi Ingia Hapa

Ningependa Kusikia Kutoka Kwako, Niandikie Hapo Chini Katika Eneo La Comment, Hii Umeipokeaje?

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii

  Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania