fbpx
Samsung, simu, Teknolojia

Samsung wamezindua Galaxy A80

samsung-wamezindua-galaxy-a80

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Moja kati ya simu ambazo zimekuwa kwenye vichwa vya habari kwa wiki kadhaa ni Samsung Glaxy A80 ambayo imekuwa ikizungumziwa sana hasa kutokana na jinsi kamerazake zilivyo.

Sasa watu wameweza kupata kufahamu undani wa rununu ambayo imezinduliwa, Galaxy A80 hivyo kuifanya Samsung kuleta simu nyingine ambayo italeta ushindani na pengine kupata soko zuri. Hii inatokana na sababu/sifa mbalimbali ambazo simu yenyewe inayo lakini kivutio kikubwa kikiwa kwenye kamera. Undani wake ni kama ifuatavyo:-

Muonekano (urefu wa kioo)/Kipuri mama.

Samsung wametengeneza simu hiyo na kufanya kioo chake kuwa na urefu a inchi 6.7 aina ya AMLED ung’avu wa kioo ukiwa 1080 x 2400px. Ukiiangalia tu rununu husika utabaini upekee iliyo nao pamoja na kutokuwa na mbwembwe za umbo la herfu “V” bado utaweza kubaini mengineyo. Upande wa kipuri mama ni Snapdragon 730 na upande wa picha ni Adreno 618.

Kamera

Hiki ndio kinachoiuza simu husika kwani kamera yake wameifanya iweze kuzunguka hivyo unaweza ukaitumia kwa ajili ya kupiga picha mbele au ukaigeza na kuwa kamera ya nyuma. Kamera kuu ina MP 48, nyingine ina MP 8 yenye uwezo wa kuzunguka nyuzi 123. Pia kuna teknolojia teknolojia ya 3D kwenye mojawapo ya kamera hivyo kuweza kuchukua picha jongefu mubashara ambazo zimeangalia sehemu moja tu (live focus videos).

INAYOHUSIANA  Uzalishwaji wa maji yaliyopo hewani! #Sayansi #Teknolojia
Galaxy A80
Muundo/mpangilio wa kamera kwenye toleo jipya la rununu familia ya Galaxy A.

Diski uhifadhi/RAM

Samsung wamefanya iwe ni simu ambayo isiwe ya kukwamakwama wakati wa ufaanyaji kazi kutokana na kuweka RAM yenye ukubwa wa GB 8 huku memori ya ndani ikiwa ni GB 128.

Betri/Mengineyo

Uwezo wa betri kwenye simu husika unavutia kwani 3700mAh sio kiwango kidogo cha nguvu ay betri pia rununu husika ina teknolojia ya kuchaji haraha kwa 25W. Inatumia Android 9 na bei yake ni $730 ambazo ni sawa na zaidi ya Tsh. 1,679,000.

INAYOHUSIANA  Fahamu Tofauti ya POP na IMAP Katika Barua Pepe!

Hiyo ndio Samsung Galaxy A80 ambayo itangia sokoni Mei 29 hivyo basi ujiandae kuinunua kwa kuiagiza au usubiri mpaka ingie nchini kwako ndio uweze kuinunua.

Vyanzo: GSMArena, Tech he Lead

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|