Simu janja zinazojichaji zenyewe kwa kutumia teknolojia ya umeme jua (solar power)? – Kama muvi vile ila ukuaji wa teknolojia unalileta jambo hili muda si mrefu katika simu tutakazonunua.
Kampuni ya utengenezaji simu ya Kyocera Corp ya nchini Japani imeonesha simu yao ambayo bado haina jina ikiwa na uwezo wa kujichaji kutumia teknolojia ya umeme jua (solar) ambayo imetengenezwa ndani ya kioo (display) chake.
Kwa sasa kwa kila chaji ya dakika tatu kupitia mwanga wa jua, utapata takribani dakika moja ya chaji ya kuongea (kupiga na kupokea simu).
Simu janja hiyo iliyotambulishwa na kampuni ya Kyocera inatumia teknolojia ya kioo spesheli cha uzalishaji umeme jua kilichotengenezwa na kampuni ya kifaransa – Sunpartner Technologies.
Kampuni ya Sunpartner imekuja na teknolojia ya kioo chembamba chenye uwezo wa kutengeneza umeme jua.
Kupitia Kioo chenye uwembamba wa ukubwa wa 0.5mm na uwezo wa kuona upande wa pili(transperancy) kwa asilimia 90, kioo hicho ambacho kinaweza kukidhi mahitaji ya teknolojia ya simu janja ambayo imeshika kasi kwa sasa bila usumbufu wowote.
Teknolojia hii imepewa jina la “Wysips Crystal”…
Ingawa teknolojia hiyo inaweza ikawa bado haijapata umaarufu kuweza kuiondoa kwenye soko la ushindani teknolojia ya hivi sasa ya kuchaji simu (the plug-and-charge) lakini inaleta ushindani mkubwa na labda makampuni makubwa ya utengenezaji simu kama vile Samsung, Huawei na wengine wanaweza fikiria kuitumia mbeleni.