Mtandao wa kijamii unaomilikiwa na Twitter wa Periscope ambao huwaruhusu watumiaji wake kuweza kurusha video za matukio mbalimbali moja kwa moja unafikiria namna ambayo watumiaji wake wataweza kuepukana na maoni ya matusi toka kwa watazamaji wao.
Matusi katika mitandao ya kijamii ni tatizo kubwa sana sio tu hapa kwetu ambako Insta ndio inaongoza lakini kwa ulimwengu mzima hili ni jambo ambalo linawaondoa watumiaji katika mitandao. Ili kuwapata watumiaji hai wengi basi mtandao ni lazima uhakikishe kwamba inapunguza kasi ya watumiaji kutukanana, hii itawafanya watumiaji kuwa huru zaidi katika mtandao na hivyo itasaidia kuongeza watumiaji hai kwa mtandao husika.
Periscope pia kama ilivyo mitandao mingine kwa muda mfupi ambao mtandao huu umetumika tayari watu wasio na utu wameanza kupeleka matusi na kurusha vitu ambavyo vita wakwera wengine, kutshugurikia hili mtandao huu unakuja na njia ambayo itawaruhusu watazamaji wa video inayorushwa moja kwa moja kuweza kuyatambua maoni yenye matusi na anayeyaandika matusi hayo atafungiwa kwa kuendelea kutoa maoni katika video hiyo ya moja kwa moja.
Periscope itawaruhusu watazamaji kuzitambua na kuripoti maoni ambayo yanamatusi ama lugha isiyopendeza baada ya kuripoti basi wao (Periscope) watahakikisha kwamba wamepeleka (maoni ambayo yametajwa kwamba yana lugha ya matusi) kwa kundi dogo la watumiaji wengine ambao nao wao watatakiwa kupigia kura kama wanakubaliana kwamba maoni hayo hayafai na iwapo itakubaliwa basi mtumiaji atazuiwa kuweka maoni yeyote mpaka baaada ya dakika moja ila kama ataendelea basi atafungiwa kutoa maoni mpaka mwisho wa video hiyo.