Akaunti yenye wafuasi wengi zaidi kuliko zote katika mtandao wa Twitter ambayo inamilikiwa na mwanamuziki wa marekani Katy Perry imedukuliwa na watu wasiojulikana ambao waliandika tweets tata kadhaa.
Katy Perry ni mtumiaji wa Twitter ambaye ndiyo anaongoza kwa wingi wa wafuasi ama followers, mwanadada huyo anawafuasi wapatao milioni 89 katika ukurasa wake wa Twitter idadi ambayo bado haijafikiwa na mtumiaji mwingine.
Akaunti ya msanii huyu ilidukuliwa na watu wasio julikana na kisha wakaweka tweets ambazo zilikuwa za kibaguzi na pia wadukuzi hao walimwandikia tweet hasimu mkuu wa mwanamuziki huyo Taylor Swift, wadukuzi hawa pia walifanikisha kuutoa wimbo mmoja wa msanii huyo ambao ulikuwa bado haujaachiwa.