fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Microsoft Teknolojia Windows

Windows 10; Kwa nini ni bora zaidi na uipate kabla muda wa BURE kuisha! #DoMore

Windows 10; Kwa nini ni bora zaidi na uipate kabla muda wa BURE kuisha! #DoMore

Spread the love

Toleo la Windows 10 limezidi kufanya vizuri, na sasa linatumika kwenye zaidi ya kompyuta milioni 300 kuanza kupatikana rasmi mwaka jana. Bado unaweza pata Windows 10 bure ila muda unayoyoma..

Kwenye makala hii nitakuonesha mambo kadhaa makuu na ya kitofauti katika programu endeshaji ya Windows 10. Hii inaweza kukusaidia kama umekuwa bado unajiuliza kama usasishe (upgrade) kompyuta yako kwenda Windows 10 au vipi.

Toleo la Windows 10 limekuja kitofauti sana, huku likiondoa mapungufu na kuzidi kuboresha vile vilivyopendwa kwenye matoleo ya Windows 7 na 8.

windows-10-kompyuta

> Microsoft Edge

Microsoft Edge ni kivinjari cha kisasa zaidi kilichochukua nafasi ya Internet Explorer. Kivinjari cha Microsoft Edge kina uwezo mbalimbali kama vile urahisi zaidi wa kusoma mambo, kuchukua ‘notes’, n.k

> Start Menu

Unakumbuka mabadiliko makubwa katika Windows 8? Wengi hawakuyapenda, hasa wanaotumia kompyuta za ‘Desktop’, kwenye Windows 10 eneo la Start Menu limerudishwa tena likiwa na maboresho kadhaa kiasi cha kuwa pa kisasa zaidi ukilinganisha na ilivyo kwenye Windows 7.

> Continuum

SOMA PIA  WhatsApp: Tumia 'Vikatuni' vya Rangi ya Ngozi Utakayo

Microsoft windows 10 simu kompyuta

Unatumia simu ya Windows 10? Kupitia teknolojia ya Continuum utaweza kuunganisha simu yako na ‘display’ nyingine kama TV na utapata muonekano wa kompyuta mara moja. Ukiunganisha na Mouse au Keyboard za ‘wireless’ na basi itakuwa imekamilika kama kompyuta. Na wakati wote huo utaweza kutumia simu yako kama kawaida.

> Kwa watengeneza apps

Je unatengeneza apps kwa ajili ya programu endeshaji za Android na iOS? Katika Windows 10 Microsoft wamehakikisha kuna mazingira yote kwa ajili ya kuweza kutumia programu endeshaji ya Windows 10 kwa ajili ya programu za ubunifu na utengenezaji apps.

> Microsoft Office 365 na apps za Office 2016

Ukuaji wa teknolojia hasa hasa za vifaa kama vile simu na tableti pamoja pia na teknolojia ya ‘Cloud’ – (uhifadhi wa data mitandaoni) umeleta faida kadhaa, na kwenye huduma ya Office 365 na apps za Office 2016 Microsoft wanaenda hatua zaidi katika kuboresha moja ya huduma maarufu sana. Kumbuka pia kwa sasa apps za Office zinapatikana kwenye ata programu endeshaji zingine za simu janja kama vile Android na iOS.

SOMA PIA  Adhabu kutokana na aina ya kosa la mtandao

Soma kuhusu Office 365 na Office 2016 – Microsoft Office 2016, Office 365 : Andika na Kusoma Mafaili Kwa Ushirikiano na Wengine

Maboresho machache kwa haraka haraka

  • Kwa kutumia teknolojia ya Cloud sasa watu tofauti wanaweza wakawa wanafanya kazi ya kuandika au kuhakiki document moja (Word, Powerpoint au OneNote) kwa wakati mmoja ata wakiwa sehemu mbili tofauti…. Upo hapo?
  • Pia Skype imeunganishwa ndani ya huduma hizi za Office na hivyo watu wanaweza kuchati n.k huku wakiwa wanafanya kazi kwenye document moja
  • Pia teknolojia ya usalama ni wa juu kuhakikisha hakuna upotevu/udukuzi wa data zinazotumiwa katika programu hizi za Office.

Je kwa nini usasishe?

Mwanzo nilisita ku’upgrade kutoka Windows 7 kwenda Windows 10 kwa muda, ila baada ya kufanya hivyo niligundua ni uamuzi bora sana nimefanya. Kwa mfano Diski C yangu ilipata nafasi huru (free space) zaidi, hii ikionesha ya kwamba ingawa Windows 10 ina maboresho kadhaa bado inachukua nafasi kidogo ya uhifadhi ukilinganisha na Windows 7.

SOMA PIA  Elon Musk wa Space X: Safari ya kwenda Mirihi / Mars kufikia 2024

Pia kumbuka ni bure kwa muda huu! – Unaupgrade kwenda Windows 10 bure bila gharama yeyote….wakati ikifika tarehe 29 Jalai mwaka huu toleo la Windows 10 litagharimu dola 119 za marekani (Zaidi ya Tsh 250,000/=). Kwa maboresho yaliyofanyika ni bora kusasisha leo badala ya kungoja zaidi.

Pia kwenye Windows 10 Microsoft wanampango wa kuendelea kuleta mambo mapya kila baada ya wakati bila kuathiri programu endeshaji hiyo. Na tayari wameahidi maboresho mapya kwenye sasisho la kuazimisha mwaka mmoja tokea toleo hilo lianze kupatikana.

Kupitia Windows 10 pamoja na huduma za Office 365 zinaonesha kwa namna gani Microsoft wanahakikisha huduma zao zinazidi kwenda na wakati na kuhakikisha zitaendelea kuwa chaguo namba moja kwa watu binafsi na makampuni kwa miaka mingi zaidi.

Je tayari umetumia Windows 10? Tuambie mtazamo wako…

Soma pia

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Comments

  1. […] Hivi sasa ni bure ku-uprade kuweka Windows 10 mpaka Julai 29 na baada ya hapo mtumiaji itamgharimu kununua programu hi…. […]

TeknoKona Teknolojia Tanzania