fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Apple IPhone simu Teknolojia

Samsung inatengenza vioo vya OLED kwa ajili ya simu janja za iPhone 13 Pro

Samsung inatengenza vioo vya OLED kwa ajili ya simu janja za iPhone 13 Pro

Spread the love

Kwa miaka kadhaa sasa umekuwepo ushirikiano kati ya Samsung na Apple hasa kwenye upande wa vioo vya OLED na kwa mara nyingine kampuni hiyo ya Korea Kusini imepata kazi kuwa sehemu iPhone 13 Pro na nduguze.

Kwa mara nyingine tena Samsung imepata tenda ya kutengeneza vioo vya OLED ambavyo vitatumika kwenye toleo lijalo la iPhone nikimaanisha iPhone 13 Pro na Pro Max. Katika hilo Samsung imeweza kupewa kazi ya kutengeneza vioo vya OLED vipatavyo milioni 80.

SOMA PIA  Energizer Power Max P18K Pop: Simu janja inayoweza kukaa zaidi ya wiki kwa kuchaji mara moja

Wakati Samsung ikiwa na kazi ya kutengeneza aina hiyo vya vioo kwa ajili ya iPhone za Apple LG na BOE wenyewe nao wamepata kazi ambapo watahusika kwenye iPhone 13 na 13 Mini. Vioo hivyo vya OLED ambavyo Samsung inatengeneza vina 120Hz ambapo hadi mwisho wa mwaka huu Samsung watakuwa wametengeneza 120 milioni, LG-50 milioni na BOE-9 milioni.

iPhone 13 Pro

Kioo cha OLED kwenye iPhone.

Mwaka huu toleo la iPhone linalokuja litatoka mwezi uliozoelekea kufuatia Samsung kwenda vizuri na utengenezaji wa sehemu hiyo ya bidhaa itakayotuika. Sasa basi tukae tayari kwa iPhone 13 na wenzake hapo mwezi Septemba mwaka huu.

SOMA PIA  Foxconn: Kazi za Wafanyakazi 60,000 zachukuliwa na Roboti! #Teknolojia

Ewe msomaji wetu kazi yako ni mojatu nayo ni kutufuatilia kila uchwao bila kujali ni siku gani kwa habari mbalimbali zinazohusu ulimwengu wa sayansi na teknolojia. TeknoKona daima inakuhabarisha.

Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania