Facebook imeamua kuleta video za moja kwa moja kwa watumiaji wake, hii inachukuliwa kama ni kujibu mapigo ya wapinzani wao Twitter ambao walileta app ya Periscope ambayo ni kwa ajiri ya kurusha video za moja kwa moja.
Facebook leo imewapatia uwezo watumiaji wake walio marekani uwezo wa kurekodi video na kuzirusha moja kwa moja, ingawa watumiaji hao hawajulishwi kwamba kuna kitu kipya kimeongezwa lakini unapoenda katika sehemu ya kuandika status yako ndio utakapoona huduma hiyo ya video za moja kwa moja.
Huduma hii mwanzoni ilikuwa kwa watu maarufu tu, baadaye ikawa kwa kurasa zilizo sibitishwa na mwisho watumiaji wa iPhone wa marekani wameweza kupata nafasi ya kutumia huduma hiyo.
Facebook wamesema katika makala ya blogu yao kwamba huduma hii inapatikana katika sehemu ya kuweka status kwa kuchagua icon ya live video ambapo utaweza kuchagua watu wanao weza kuiona video hii. Inapo anza kwenda hewani unaweza kuona watu wanaoiangalia na pia kuona comments zao. Ukimaliza kurusha video hii itawekwa kwatika ukurasa wako na marafiki zako wataweza kuicheza baadae.
Hii ni nafasi kwa makampuni kuweza kujitangaza kwa kutumia video za moja kwa moja lakini pia ni nafasi ya watumiaji wa kawaida kuwapamoja na marafiki zao. Ingawa huduma hii itawafaa watu wenye intaneti yenye kasi na vifurushi vikubwa lakini bado tunaaamini itakapo kuja hapa kwetu Afrika Mashariki itapata watumiaji wengi.
One Comment