fbpx

LI-FI – Teknolojia Itakayo badili Ulimwengu wa Teknolojia na Mawasiliano

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Li-Fi ni  teknolojia  itumiayo miale ya mwanga kusafirisha  data(visible light proton). Teknolojia hii ya mawasilano husafirisha data katika spidi ya juu mara 100 zaidi kulinganisha na teknolojia ya Wi-Fi itumiayo mawimbi ya redio(radio waves).

Teknoljia hii itamuhitaji mtumiaji kuwa na kifaa maalumu cha kupokea mwanga ( led bulb),kifaa cha kutambua mwanga na Munganisho intaneti kutumia teknolojia hii.

Uvumbuzi huu wa kihistoria ulifanywa na Prof Harald Haas ambaye sasa ni mkurungezi mtendaji wa kampuni ya PURELIFI  inayoshughulika na utoaji wa huduma za mfumo huu wa mawasilano. Uvumbuzi huu umejaribiwa na kuthibitika kufanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu. Teknolojia hii hutumika katika vifaa vyote viwezavyo kuunganishwa na intaneti kama Simu, Kompyuta, Tv na vingine.

INAYOHUSIANA  Google na Microsoft waungana katika vita dhidi ya mitandao ya mafaili ya wizi

Prof  Haas aliushutua ulimwengu wa teknolojia pale alipoitambulisha  teknolojia hii ambayo sasa lifi inaweza kusafirisha data mpaka kwa spidi ya GB Moja kwa sekunde 1GbPs lakini inasemekana kuweza kufikia 224GbPs. Yaani itakuwezesha kudownload muvi yenye ukubwa wa Gb 1 kwa sekunde  moja tu.

Li-Fi-610x419

Faida kubwa za utumiaji wa teknolojia hii ni kwamba  kwanza amna muingiliano wa signal hivyo itakuwa na manufaa makubwa  kama  itatumika katika sehemu ambazo  mwingiliano wa signals ni tatizo kama  katika ndege. na pili kutakuwa na usalama kwa mtumiaji zidi ya udukuzi  kwani miale hii haiwezi kupitiliza katika ukuta

teknolojia ya lifi

teknolojia ya lifi

Ingawaje teknolojia hii haitafanya kazi pale kifaa kitoacho mwanga led bulb kitakapozimwa hivyo bhasi bhasi itamulazimu mtumiaji kuwasha taa muda wote. Uzuri ni kwamba taa zitakazo tumika katika lifi zimetengenezwa kwa mfumo wa hali ya kiasi cha kwamba inaweza kuwaka bila kutoa mwanga uonekanao.

INAYOHUSIANA  Apple Kuja Na Emoji Mpya Katika Vifaa Vya iOs na macOS!

li-fi-vs-wi-fi-610x359

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Leave A Reply