Huduma za Augmented Reality (AR) na Virtual Reality (VR) zinaendelea kupewa kipaumbele sana katika dunia ya sasa na Apple nao bado hawajasalia nyuma.
Ni wazi kuwa tulikua tukisikia kuwa Apple inapambana sana kuhakikisha kuwa inaleta sokoni kifaa au vifaa ambavyo vinatumia teknolojia hiyo.

Kutokana na taarifa ambazo zimetoka na sio rasmi sana inasemekana kwamba vifaa hiyo vinaweza anza toka mwezi januari mwaka 2023.
Unaweza ukawa unajiuliza mfumo wa vifaa hivi utakuaje? Kwa haraka haraka ni kwamba vifaa hivi vitakua ni vipya kabia kwa Apple
Yaani sio simu wa iPad wa Mac bali vitakua ni vifaa vile vya mfumo wa ‘helmet’ –zinazofunika macho—zikiwa na teknolojia hii ya AR/VR.

Kwa sasa makampuni makubwa kama Meta na mengine mengi yanapambana sana katika kuleta teknolojia ya aina hii.
Kumbuka na teknolojia hii katika soko inakua kwa kiasi kikubwa sana, na hii ni moja ya njia inayofanya makampuni mengine kuwekeza vikubwa katika teknolojia hii
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je uko tayari kuanza kutumia teknolojia hii?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.