Teknolojia ya magari yanayotumia umeme (electric cars) imezidi kushika umaarufu katika nchi nyingi zilizoendelea, na kutokana na hili kuna harakati mbalimbali zinafanyika kuzidi kuwafanya watu wengi wanunua magari yanayotumia teknolojia hiyo na kuachana na yanayotumia mafuta.
Kwa muda mrefu juhudi nyingi zimekuwa ni kuona jinsi ya kuboresha uwezo wa chaji wa mabetri yake na uharaka wa kuyachajisha pale panapoitajika. Kumbuka inachukua muda mfupi zaidi kujaza mafuta tenki nzima wakati inaweza kuchukua masaa kadhaa kuchaji betri la gari linalotumia umeme.
Pia kwa wastani gari lilojazwa mafuta tenki nzima lina uwezo wa kusafiri umbali mrefu zaidi bila kuongeza mafuta ukilinganisha na lile linalotumia umeme. Kutokana na hili shirika linalosimamia barabara za nchini Uingereza limejikita katika utengenezaji wa barabara spesheli zitakazokuwa zimeunganishwa na gridi ya umeme na kupitia vifaa spesheli vitakavyowekwa kwenye barabara na kingine chini ya magari yanayotumia umeme – basi betri za magari hayo zitakuwa zinapata umeme na kujichaji kila zinapokuwa zinapita katika barabara hiyo spesheli.
Uhamishaji huo wa umeme wa bila kushikanisha chochote, yaani ‘wireless’ utategemea utumiaji wa teknolojia ya ‘electronic magnetic.
Serikali ya Uingereza imetenga utumiaji wa takribani Tsh Trilioni 1.6 katika kuwezesha utengenezaji wa barabara hizo ndani ya miaka 5.
Teknolojia ya magari yatumiayo umeme badala ya mafuta ya petrol au diseli katika uendeshaji wa injini za magari imejipatia umaarufu sana katika kipindi cha miaka hivi karibuni. Wapenda mazingira wakiisifu zaidi kwani haisababisha uchafuzi wa mazingira na pia watu wanaongalia miaka ya mbele wakisema ni jambo zuri kwani wanaamini mafuta kuna miaka yataisha kabisa na hivyo ni bora kuanza kuangalia katika teknolojia mbadala.
Soma Pia – Barabara ya Sola Yafunguliwa Uholanzi
Je una maoni gani katika hili? Endelea kutembelea mtandao wako namba moja kwa habari na maujanja ya kiteknolojia katika lugha ya kiswahili.
No Comment! Be the first one.