fbpx

Huawei yaizidi Apple kimauzo

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Ushindani kwenye biashara ni lazima na kwa mwaka 2018 Apple haina rekodi nzuri sana ukilinganisha na wapinzani wake wakuu na hii inadhihirika kwa mara nyingine tena Huawei kuweza kuizidi kampuni nguli kimauzo.

Katika hatua za kufunga hesabu za mwaka husika Huawei imeweza kuwa mbele ya Apple kwenye mauzo ya jumla kwa bidhaa zake ambapo yameonekana kuimarika kutokana na simu Huawei P20 huko Uchina, Ulaya na Afrika.

Huawei imeweza kushika nafasi ya pili nyuma ya Samsung huku Apple ikishika nafasi ya tatu. Mauzo ya jumla kwa bidhaa za Huaei yameweza kufikia 200 mil. (sawa na ongezeko la 30%) ukilinganisha na 153m mwaka 2017.

kimauzo

Orodha ya makampuni yaliyofanya vizuri katika mwaka 2017-18.

Ingawa Huawei wameweza kufanya vizuri kiujula lakini bidhaa zao hazipaswi kuuzwa nchini Australia, Canada na Marekani.

Vyanzo: GSMArena, Phone Arena

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Samsung Imesema Itazidi Kuwa Namba 1 Kwa Miaka Mingine 10!
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.