Ni miezi mingi imepita tokea huduma ya WhatsApp kwenye kivinjari (browser) cha kompyuta kuja kwa watumiaji wa simu za Android, BlackBerry na Windows, na sasa baada ya muda mrefu huduma hiyo itawezekana kwa watumiaji wa simu za iPhone zinazotumia programu endeshaji ya iOS.
Timu ya WhatsApp kwa muda mrefu ilisema teknolojia hiyo inachelewa kwa watumiaji wa simu za iPhone kutokana na ugumu uliowekwa na watengenezaji wa programu endeshaji ya iOS yaani kampuni ya Apple. Na sasa inaonekana waliweza kushirikiana na kufanikisha kutatua.
Kama wewe ni mtumiaji wa iPhone basi nenda kwenye soko la apps la ios, yaani App Store na usasishe (update) app yako ya WhatsApp. Uwezo haujaanza kupatikana kwa watumiaji wote wa iOS ila taratibu unatambaa kwa wengi zaidi hivyo hakikisha unaangalia mara kwa mara.
Huduma ya WhatsApp kwenye kivinjari cha kompyuta itakuwezesha kupokea, kusoma na kujibu ujumbe unaoingia kwenye WhatsApp ya simu yako moja kwa moja kwenye kivinjari cha kompyuta yako bila kushughulika na simu yako. Kinachotakiwa ni simu yako tuu kuwa kwenye huduma ya intaneti kama kawaida.
Hatua
1. Kwenye kompyuta yako, fungua Google Chrome kisha nenda https://web.whatsapp.com
2. Utaona kodi ya QR
3. Fungua app ya WhatsApp, Nenda ‘Settings’, Chagua ‘WhatsApp web’.
4. Oneshea kamera ya simu kwenye eneo lenye code ya QR kwenye kivinjari chako, WhatsApp yako itaunganishwa mara moja na utaweza kutumia huduma ya WhatsApp kwenye kompyuta yako mara moja
Je unatumia simu ya iPhone na umekuwa unasubiria kwa hamu uweze kutumia WhatsApp kwenye kivinjari? Furahia sasa. Huduma ya WhatsApp for Web inapatikana katika vivinjari vya Chrome, Firefox na Opera.
No Comment! Be the first one.