Mfumo wa teknolojia inayotuwezesha kutumia Emoji katika simu zetu upo njiani kupitia na kuthibitisha ongezeka la Emoji nyingine 38 katika teknolojia hiyo. Na Emoji hizo mpya zitakuwa ni tamu kweli kweli.
Shirika linalosimamia mambo ya Emoji, linafahamika kwa jina la Unicode Consortium , ndilo linalosimamia maendelea na marekebisho ya teknolojia ya Unicode 9 ambayo ndio inatumiwa katika simu janja zetu kuwezesha utumiaji wa Emoji. Shirika hilo limepokea Emoji mpya 38 ambazo zinategemewa kuanza kusambazwa kwa watengenezaji programu endeshaji za simu (Android, iOS, n.k) na kuwezesha Emoji hizo mpya kuanza kutumika kufikia kati kati ya mwaka 2016.
Je kuna nini kipya?
Bwana Harusi!
Kulikuwa tayari na Emoji ya bibi harusi na sasa bwana harusi pia anaongezwa.
Mshikaji anayecheza muziki
Tayari kulikuwa na emoji ya binti anayecheza muziki na hakuna ubishi saa nyingine ata sisi wanaume tunataka kutuma emoji ya kucheza tukimaanisha washikaji wajiunge nasi viwanja…ondoa hofu, tutakuwa na emoji yetu pia.
Mke wa Santa/Baba Krismasi
Tayari kulikuwa na Emoji ya Santa mwanaume, na sasa kutakuwa na emoji ya mke wake pia
Mtoto wa Kiume wa Mfalme (Prince)
Tayari kulikuwa na emoji ya binti wa mfalme na sasa kutakuwepo na nyingine spesheli kwa ajili ya wakaka
Mjamzito
Wadada ondoeni shaka, hamtaitaji kuandika maelezo mengi kusema ya kwamba wewe ni mjamzito… kutakuwa na emoji spesheli inayopunguza urefu wa maneno. 🙂
Sura zaidi
Je sura zilizopo kwenye emoji za sasa hazitoshi kuelezea kila kitu? Basi ondoa shaka, kuna sura nyingine mpya zitaongezwa.
Alama za Vidole
Tushukuru bado ile emoji ya kidole cha kati inayoombwa na wengi bado hawajaifikiria kuiweka. Hizi ndizo alama za vidole unazoweza kuzitumia muda si mrefu.
Usafiri
Kuna Emoji zimeongezwa kwa ajili ya kuonesha vyombo vingine vya usafiri
No Comment! Be the first one.