fbpx

Oppo A5s: Oppo wana toleo jipya la simu

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

ICT CONFERENCE 2019

Sambaza

Katika moja ya makampuni ambayo yanaleta ushindani dhidi ya wakongwe ni Oppo ambapo kiujumla bidhaa zao zimekuwa zikikubalika na kuifanya kampuni husika kuwa kwenye nafasi za juu kiushindani na siku si nyingi zilizopitawametoa Oppo A5s.

Oppo imekuwa ni zile kampuni ambazo zinayoa simu janja mara kwa mara; inawezaikawa ni muendelezo  wa toleo fulani au ikawa ni rununu ambayo ni kutoka familia mpya kabisa. Kwa Oppo A5s ni muendelezo tu wa iliyomtangulia (Oppo A5) na kimsingi tofauti kati ya simu hizo ni kwenye baadhi ya vipuri.Simu hii ambayo naiangazia leo kwa jina lingine inafahamika kama “AX5s” na sifa zake ni kama ifuatavyo:-

INAYOHUSIANA  WhatsApp na Gmail, na apps 6 zingine zenye Watumiaji Bilioni moja na zaidi kwa Mwezi

Kipengele

Maelezo

Kipuri mama+Ufanisi Mediatek MT6765 Helio P35, vipuri nane (8) vyenye kasi ya 4×2.3 GHz Cortex-A53 na 4×1.8 GHz Cortex-A53,

Kipuri kinachofanya ung’avu wa picha ni PowerVR GE8320

Kioo+muonekano Kina chake ni aina ya IPS urefu wa inchi 6.2 (720 x 1,520px). Kwenye uso wa mbele ina duara dogo lililoizunguka kamera ya mbele
Kamera Kamera ya nyuma: MP 13+MP 2

Kamera ya nyuma: MP 8

Oppo A5s

Muonekano waOppo A5s

Kipengele

Maelezo

RAM+Diski uhifadhi

Ina GB 3 za RAM, GB 64 memori ya ndani lakini pia inawezekana kuongeza memori ya ziada mpaka GB 256

Betri+Programu endeshi

Betri yake hatoki na ina 4320mAh, imewekwa Android 8.1 Oreo kama programu endeshaji

Rangi+Mengineyo

Ipo katika rangi Nyekundu na Nyeusi. Inatumia teknolojia ya alama ya kidole, ina sehemu ya kuchomeka spika za masikioni, redio, Bluetooth, Wi-Fi, inatumia USB OTG

INAYOHUSIANA  Hii ndio simu janja ya kwanza yenye mkunjo

Bei na kuhusu lini itaingia sokoni ni vitu amabavyo bado havijafahamika na kimsingi Oppo wameendelea kuleta simu zenye uborawa kati ambazo huenda isiwe ghali kuipata. Wewe unapenda bidhaa za Oppo?

Facebook Comments

Sambaza

ICT CONFERENCE 2019

Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.