fbpx

Vespa ya umeme kuuzwa mwezi Oktoba

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Pikipiki ya kwanza, Vespa inayotumia umeme iliyotayarishwa kwa muda mrefu inatarajiwa kuanza kuuzwa mwezi Oktoba mwaka huu.

Uuzwaji huo unatarajiwa kuanza mwezi ujao na soko la kwanza litakuwa  kwa bara la Ulaya ambapo masoko ya Marekani na Asia yatakuwa kuanzia mapema mwaka 2019.

Kampuni inayohusika na utengezaji wa bidhaa hiyo, Piaggio Group bado haijaweka wazi bei ya Vespa lakini itauzwa kwa kiwango cha kawaida.

Pikipiki hiyo ya umeme itakuwa na uwezo wa kwenda Kilomita 100 (sawa na maili 62) ikiwa na nguvu zaidi kuliko Vespa ya kawaida yenye 50cc.

Vespa itahitaji kuchajiwa upya baada ya kutumika kwa saa nne. Mbali na hapo betri hiyo itaanza kupungua nguvu kwa kuchajiwa mara kwa mara baada ya miaka 10 ya kutumika kwa asilimia 80.

Vespa ya umeme

Pikipiki ya kwanza iitwayo Vespa inayotumia umeme.

Haitakuwa na sauti inapoendeshwa ila itakuwa inatambua sehemu za wapita kwa miguu pamoja na kupishana kwa magari barabarani.

Historia kidogo……

Kampuni ya Piaggio yenye makao makuu yake nchini Italia ilianza kuzalisha Vespa tangu mwaka 1946 na zimekuwa maarufu kwa watu wengi wanaopenda usafiri wenye kasi ya kawaida isiyo hatarisha usalama wa mtumiaji.

Vespa ya umeme

Hiyo ndio pikipiki ya kwanza iitwayo VESPA.

Kampuni ya Piaggio pia ina mpango wa kutoa Vespa  ya umeme yenye uwezo zaidi ya hii ya sasa.

Haijaelezwa rasmi kasi yake lakini bila shaka itakuwa kwa kilomita 30 kwa saa ili kuwa na uwezo wa kuhifadhi maisha ya Betri yake.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Simu za Orange Klif za TShs 75, 000 Kuja kwanza Kenya Kwa Afrika Mashariki
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.