Saa nyingine kuchagua simu ambayo ina uwezo mkubwa katika swala zima la kamera haimaanishi kuwa ndio utakua unapiga picha nzuri tuu. Ukiwa na usaidizi wa App kadhaa unaweza ukawa unapata picha nzuri zadi
Kama unakumbuka tulishawahi kuandika Juu ya App Bora Kwa Ajili Ya Kamera Za Android Na iOS!
Leo tuangalie katika vifaa vya Android, ni App gani ambazo zinaweza zikakufanya uwe na ukakika wa kupiga picha nzuri katika simu janja yako.
Moja Kwa Moja Tuzifahamu App Hizo.
1. Camera 360

Licha ya App hii kuwa imependekezwa na watu wengi bado ina watumiaji wengi. Watu zaidi ya milioni 400 wanatumia App hii. Kila kitu katika App hii utakipenda kuanzia HDR na Kadhalika. App hii ina zaidi ya Filter 200 na ‘Effect’ kadha wa kadha ambazo kwa namna moja au nyingine ukizichagua kwa umakini unaweza ukapata picha nzuri.
Ndio Google wana kamera pia (hahaa)!. Google hawajawahi kufanya makosa katika App zao, sioni sababu ya kutoikubali App wakati imetengenezwa na Google. Hapa App ya Cardboard Camera ni ya aina yake pia. Katika simu yako unaweza ukatumia ‘Effect’ kama vile Lens Blur (hii inakusaidia kuweka ukungu katika sehemu ya picha na kuacha sehemu nyingine ionekane vizuri). Ukiachana na hayo kuna vitu vingine vingi unavyoweza fanya ili kupendezesha picha yako.
3. Camera MX.

App hii ni ya bure katika soko la Google play, mpaka sasa imeshashushwa zaidi ya mara milioni 10. ‘Effect’ zilizopo katika App hii ni kama vile HDR, Lomo, Mirror (kioo), Overlay na nyingine kadha wa kadha. Uzuri wa App hii ni kwamba pia inakuruhusu kuhariri video kwa kutumia kifaa chako.
4. GIF Camera.

App hii ni moja katika ya App bora za kamera duniani, kama jina lake linavyosema hapa unaweza ukapiga picha mbalimbali na kuzihifadhi katika mfumo wa GIF (ule mfumo wa kufanya picha zicheze cheze)
5. Cymera .

Hii pia ni bora na ina zaidi ya watumiaji milioni 150 duniani. Ukiachana na kujikita katika swala zima la kamera pia ni sehemu ambayo inaweza ikatumika katika kuhariri picha zako. Baada ya kuhariri picha zako unaweza ukaamua kuziunganisha na kisha kuzituma katika mitandao yako ya kijamii.

Kama jina linavyojieleza ndio App hii ilivyo. Ukiwa katika App hii unaweza kuchagua ni jinsi gani unataka kuchagua upigaji wako wa picha. Uwezo wake wa panorama ni wa nyuzi 360 (inamaanisha hakuna eneo ambalo utaliacha ukiachana na hayo kuna mengine mengi tuu
Kabla watu wa iOS hamjaanza kutaka kunikasirikia someni hapa mtapata kitu!