Habari nzuri kwa watumiaji wa simu za Samsung Galaxy S6 na Galaxy S6 Edge kwani muda si mrefu wataweza kupata msasisho (update) wa Android 6.0.1 Marshmallow.
Kwa sasa kampuni hiyo ishaanza kuanza kutoa msasisho huo wa toleo jipya kabisa la Android kwa watumiaji wa Samsung Galaxy S6 na Galaxy S6 Edge wa nchini Korea kusini. Kwa mara nyingi kampuni ya Samsung huwa inaanza kutoa masasisho katika taifa hilo ambalo ndio nyumbani kwao.
Ingawa badi hawajatoa ratiba rasmi ila ni kawaida ya masasisho kuanza kusambaa kwa watumiaji wa mataifa mengine wiki kadhaa baada ya watumiaji wa nchini Korea Kusini kupata masasisho.
Kuanza kutoa masasisho katika nchi moja tuu huwasaidia kuona matatizo na kuyarekebisha kabla ya kuanza kuyasambaza kwa watumiaji wa simu husika duniani kote.
Ni nini kipya kwa toleo la Android 6.0.1 Marshmallow kwa watumiaji wa Samsung Galaxy S6 na Galaxy S6 Edge?
Haya ni baadhi ya kuyatarajia…
- Upya utarajiwe baada ya kusasisha simu yako.
- Hii ni pamoja na mabadiliko kidogo ya kimuonekano katika eneo la ‘Status Bar‘
- Menu utakayoiona baada ya kubofya kitufe cha kuzima simu (power menu) nayo imafanyiwa mabadiliko kidogo
- Pia baadhi ya mionekano ya App Icons imebadilishwa kidogo
- Pia kutakuwa na emoji mbalimbali mpya
Soma Pia – Uchambuzi wa Samsung Galaxy S6 na Galaxy S6 Edge
Kama wewe ni mtumiaji wa simu hizi basi endelea kuwa na subira na muda si mrefu kupitia eneo la ‘Update’ kwenye simu yako utaweza kuona mualiko wa kusasisha (update).
Vyanzo: Mbalimbali mtandaoni
No Comment! Be the first one.