fbpx
apps, Google, Teknolojia

Ruhusu Google kufuta kirahisi vitu

uwezo-wa-watu-kufuta-yale-yanayofanyika-kwenye-google
Sambaza

Ahsante kwa teknolojia kwa kurahisisha vitu kutokana na kwamba tunaweza kufahamu vingi wakati wote/mahali popote na hasa kupitia huduma mbalimbali za Google ambazo zinatusaidia katika maisha yetu ya kila siku kwa namna moja au nyingine katika kuhakikisha shughli zinafanyika.

Ulinzi/usalama wa vile vitu ambavyo tunafanya kila siku kupitia ifaa vya kidijiti, mitandao ya kijamii, n.k imekuwa ni suala ambalo makampuni mbalimbali yakitafuta mbinu mbalimbali kuhakikisha kwamba inalinda data za watu kupitia huduma zao mbalimbali mathalani jinsi ya kufika sehemu fulani kwa ramani, soko la programu tumishi kwa Android, n.k.

Google wajihami kuhusu kufuta data.

Katika hali ya kufanya data za watu zinaondolewa na pengine kutotumiwa vibaya Google wameweka wazi kuwa wataongeza kipengele ambacho kitaweza kufuta zile sehemu ulizotafuta kwenye huduma zao baada ya muda fulani kupita.

Tunafahamu kuwa unapotumia programu ya “Ramani za Google”/chochote tunachofanya kwenye Google vitu vyote vinakuwa vimehifadhia kwenye historia sasa data hizo zitaweza kufutika baada ya miezi mitatu (3) au kumi na minane (18) kupita.

kufuta
Google waongeza uwanja mpana watu kuweza kufuta data zao.

Hivyo ndivyo Google wanafanya katika kuhakikisha data zako zinaondolewa kwenye macho yako au machoni pa watu ingawa unaweza ukachagua ukawa unazifuta mwenyewe kama hutopenda zijifute zenyewe baada ya muda fulani kupita.

Chanzo: GSMArena

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Helios Towers, wamiliki na waendeshaji minara Afrika sasa kwenye soko la hisa Uingereza.
0 Comments
Share
Tags: ,

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|