fbpx

ALPHABET, Google, Teknolojia

Tetesi; App ya Google Allo kuja wiki hii

tetesi-app-ya-google-allo-kuja-wiki-hii

Sambaza

Zipo tetesi katika mitandao ya teknolojia kwamba kampuni ya Google ipo mbioni kuachia app yake mpya ya Allo ambayo ni kwaajiri ya kutuma ujumbe ambayo ilitangazwa katika mkutano wa waandaji Google I/O uliofanyika mwezi Mei mwaka huu.

Google Allo
Picha ya muonekano wa app hiyo katika simu.

Google Allo ni app kwaajiri ya kuchati kama vile zilivo app za Hangouts na messenger ambazo pia zinatengenezwa na Google lakini app hii inakuja na uwezo maalumu wa kujifunza tabia yako na namna unayojibu meseji zako hivyo kukusaidia kujibu meseji.

google-allo
Picha nyingine ikionesha namna app hii itakavyokuwa inafanya kazi.

Allo itakuja na uwezo wa mkubwa wa kujifunza kile tabia zako za uandishi wa ujumbe, utalaamu huu ambao kwa kingereza unaitwa Machine learning unaifanya app hii kujifunza namna ambayo unajibu jumbe zako na hivyo baada ya muda mrefu wa kujifunza itaweza kujibu baadhi ya meseji kutoka kwa marafiki zako bila wewe kuandika kitu.

Google allo hata hivyo ni wazi haitaelewa lugha isiyo rasmi hii ni pamoja na kiswahili ama kingereza kisicho rasmi yaani lugha ya ufupisho ambayo inatumika zaidi katika mitandao. Kwa mtazamo wa haraka haraka app hii itapata shida kufikia malengo kwa watumiaji vijana wa karne hii.

INAYOHUSIANA  HP kulipwa takribani trilioni 6.6 za Tsh na Oracle baada ya kushinda kesi

Hii ni changamoto kwa waandaaji wa app na programu za kompyuta kuangalia katika eneo la Machine learning na kulifanyia kazi eneo hili la sekta ya teknolojia.

google allo
App hii imepewa nyota 4.9 na wale walio ijaribu na kutoa mrejesho wao.

Wegi wanasubiria hii app kwa hamu ili kujionea ni kiasi gani inaweza kuwa na msaada  hasa kwa watumiaji wa kawaida! Tayari app hii imepewa nyota 4.9 na walio ijaribu katika soko la Google play kama inavyoonekana katika picha hapo juu.

INAYOHUSIANA  Uraibu wa kutumia kompyuta: Serikali ya Korea Kusini yapata suluhisho

Je tuambie unadhani app hii itakuwa na mashiko? ama itakuwa POGBA tu?????

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: , ,

Nickson