fbpx

Apple, IPhone, simu, Teknolojia, Uchambuzi

Ujue undani wa iPhone XS Max

ujue-undani-wa-iphone-xs-max

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Sambaza

Moja kati ya simu ambazo ni ghali mpaka hivi leo tangu kutoka kwake basi iPhone XS Max na hili pengine linasababishwa na vilivyomo kwenye rununu lakini inajulikana bidhaa za Apple bei zake huwa zipo juu.

Leo msomaji wetu wa TeknoKona tutakuangazia simu mpya ya iPhone XS Max yenye sifa kadhaa za kupendeza. Kwa lugha nyingine, simu hii inafahamika kama ni iPhone ‘Ten S‘ Max, na siyo ‘Excess Max‘, lakini hivyo ndivyo watu wengi wanavyoweza kutafsiri jina lake.

>Kwanza, ina skirini ya ukubwa wa inchi 6.5 iliyo na betri kubwa zaidi pia, pamoja na sifa zote zilizomo katika simu ndogo zaidi za iPhone XS kama kuwa na laini mbili za simu, kamera ya kisasa na bora zaidi na pia kuwa na prosesa yenye kufanya kazi kwa kasi kubwa ijuliknayo kama ‘Super-fast A12 Bionic processor’ na vilevile, ina shajara mpya ya kuhifadhia taarifa yenye ukubwa wa GB 512.

iPhone XS Max

 

Vipimo vya iPhone XS Max ni milimita 157.5 x 77.4 x 7.7, hivyo kuwa sawa na ukubwa wa Samsung Galaxy Note 9, ambayo kwa ujumla huja katika vipimo vya 161.9 x 76.4 x 8.8mm. Hii ni simu kubwa, na hakuna namna unayoweza kuitumia kwa mkono mmoja.

Cha kushangaza, ingawa iPhone XS Max kiasi ni nzito kuliko Galaxy Note 9 (gramu 208 dhidi ya gramu 202), mkononi huonekana kuwa nyepesi zaidi ya wapinzani wake.

Kwa maneno mengine, iPhone XS Max inaonekana kama simu kubwa na nzito zaidi, lakini utashangaa wakati ukiikamata. Kama ilivyo kwa simu nyingine za modeli za iPhone X, kimsingi simu ya iPhone XS Max ina vioo viwili vilivyounganishwa na kwa fremu ya chuma imara.

iPhone XS Max
Apple inadai kwamba imetumia vioo imara kuliko vyote vilivyopo kwa sasa kwa ajili ya matumizi ya simu za rununu, na hakitelezi sana kama wengi walivyotaraji.

Kioo

Kitu cha kuvutia zaidi kwa yeyote kuhusiana na simu za iPhone XS Max ni skirini (Kioo) yake ya OLED, ambayo kwa ufupi tu ni kwamba inavutia kwa kuwa kwake kubwa zaidi kuliko simu zote zilizowahi kutolewa na Apple.

INAYOHUSIANA  Ujio wa AirPods Pro 2020 wasogezwa mbele

Apple wanadai kwamba skirini yake kwa sasa ina asilimia 60 ya umbali wa kunyumbulika, hivyo kuzifanya picha/picha za mnato kuwa bora zaidi.

Kamera

Kamera ya iPhone XS Max ina ubora wa hali ya juu ikiwa na ziada ya kuwa na lenzi mbili, lakini Apple wameiongezea madoido kwa kuifanya kuwa na sensa mbili za 12MP kwa nyuma, na pia ukubwa wa pixel sasa umeongezwa maradufu hadi kufikia ukubwa wa 1.4um kwa kamera ya upana.

iPhone XS Max
Uwezo wake wa kuwa na laini mbili na mashine (processor) inayofanya kazi kwa kasi kubwa ya A12 Bionic, Apple inaonekana kuzalisha bidhaa bora zaidi inayofunika nyingine zilizopita.

Memori/Bei

Toleo hilo litakuwa sokoni kwa ukubwa wa GB 64, GB 256 na GB 512, na RAM ni GB 4. Bei yake ni kuanzia $654|zaidi ya Tsh. 1,504,200 bei ya ughaibuni na yenye memori kubwa kabisa (GB 512) ni $738|zaidi ya Tsh. 1,697,400.

INAYOHUSIANA  Kilimo kinachotumia teknolojia zaidi

Mengineyo

>iPhone XS imewekwa katika daraja la IP68, hivyo ikimaanisha kwamba haiwezi kuingia maji ikitumbukizwa kwenye maji ya kina cha mita mbili na kuachwa humo kwa dakika 30.

>Kadhalika, simu za iPhone XS Max zitakuwa na chaguo la rangi tatu: kijivu laini na fedha zikirudi tena, huku mpya ikiwa ni matoleo ya rangi ya dhahabu ambayo huifanya ionekane ya kuvutia zaidi, hasa kutokana na uwapo wa chuma cha kung’ara kuizunguka simu hiyo.

>Pia ina uwezo wa kuchajiwa bila kutumia waya kama ilivyo kwa betri za sasa za iPhone, zikiwa ni zile zenye mfumo wa kiwango cha Qi.

Vipi imekuvutia? Una lipi la kutushirikisha kuhusiana na simu hiyo? Usisite kutufuatilia kila wakati kupitia mitandao ya kijamii.

Chanzo: GSMArena

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Sambaza

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.