fbpx
apps, Teknolojia

Wanaolipia Spotify wafikia milioni 100

wanaolipia-spotify-wafikia-milioni-100
Sambaza

Katika dunia ya leo mtindo wa kusikiliza/kangalia picha jongefu bila kuihifadhi ni kitu cha kawaida sana hasa ukiwa na intaneti ambayo ina kasi ambapo ukiangalia kitu hakikwami (kusubiri kwa sekunde kadhaa ndio uweze kuendelea) hapo ndipo mtoa huduma kama Spotify anapofahamika.

Spotify ni nini?

Hii ni tovuti/programu tumishi inayopatikana kwenye iOS/Android ambapo inatoa huduma ya kuweza kusikiliza au kuweza kupakua mamilioni ya nyimbo/picha mnato kutoka kwa wasanii mbalimbali duniani wenye kazi zao huko. Huduma hii ni BURE kwa baadhi ya huduma lakini kama unataka kupata raha zaidi mathalani kuweza kushusha wimbo/nyimbo au picha jongefu unalipia $9.99|zaidi ya Tsh. 23,000 kwa mwezi.

Wanaolipia Spotify
Nyimbo mbalimbali zinazopatikana ingawa kwa wanaolipia Spotify wnnapata mengi zaidi.

Ikiwa tumeshaanza robo ya pili ya mwaka 2019 makampuni mengi tuu duniani yameweza kuweka wazi faida/hasara waliyopata katika kipindi cha miezi mitatu nyuma (Jan-Apr) na kwa Spotify wanaonekana kupata hasara ya karibu $159 milioni katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita kulinganisha na faida ya zaidu ya 4494 mil. katika kipindi sawa na hicho mwaka jana.

INAYOHUSIANA  Simu ndogo unayoweza 'Kuizungushazungusha'

Hata ivyo, Spotify wameweza kufikia kupata wateja milioni 100 kwa idadi ambao wanalipia kuweza kufurahia huduma zinazopatikana kwa kuchangia ada ya kila mwezi. Mafanikio hayo yamechagizwa na wateja wa India ambapo karibu watu milioni moja waliweza kujiunga na huduma ya kulippia katika wikiendi ya kwanza ilipopekekwa huko kipindi cha robo ya nne mwaka 2018.

Wanaolipia Spotify
Wateja wanaolipia kupata huduma ya Spotify wafika mil. 100.

Kwa ujumla mpaka sasa Spotify ina wateja milioni 117 (wanaoalipia na wasiolipia), washindani wake wakuu ni Apple Music, Tidal, Youtube. Vipi na wewe ni mmoja wa wateja wa kulipia ndani Spotify?

Chanzo: GSMArena

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|