Jinsi Ya Kuweka ‘Dark Mode’ Katika Gmail! #Android #iOS #Kompyuta

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Teknolojia ya ‘Dark Mode’ imetawala sana siku hizi, makampuni mbali mbali yanapambana kwa kina ili kuendana na teknolojia hii

Tumeona pia katika OS mbalimbali zinapamba vikali ili kuhakikisha zinakuwa na huduma hii, ukiana na OS hata Apps mbali mbali tunaona zinajifua vikali katika kuhakikisha zinakuja na sifa hii.

Leo TeknoKona inakuletea maujanja juu ya kufanikisha hili katika vifaa vyote

  1. Gmail ‘Dark Mode’ Kwa Ajili Ya Kompyuta

Bila kusema mengi ingia katika akaunti yako ya Gmail na nenda moja kwa moja katika ‘Settings’ kwa upande wa juu pale chini ya picha profile yako.

Gmail Dark Mode Kompyuta

Kisha chagua ‘Theme’  kuna picha picha nyingi zitatokea na kasha chagua ile ambayo ina rangi nyeusi tuu. Ukiweza fanya hivyo  utakua umeliwezesha hilo.

  1. Gmail ‘Dark Mode’ Katika Kifaa Cha Android
INAYOHUSIANA  Samsung watoa masasisho ya Android Pie kwenye Galaxy J7 Duo

Cha kwanza kabisa hapa inabidi uhakikishe una toleo jipya la App ya google kama bado nenda katika playstore na kasha sasisha (update).

Kama una Android 10 katika kifaa chako hauna haja ya kutaka jasho sana kwani huduma ya ‘Dark Mode’ itawezeshwa moja kwa moja. Au kwa hali nyingine unaweza  kwenda katika menu ukiwa ndani ya App ya Gmail na kisha ukaenda katika ‘Settings’  kisha ‘General Settings’  hapo unaweza ukabadilisha ‘Theme’ unayotaka na chaguo la ‘Dark Mode’ lipo humo humo.

Gmail Dark Mode Katika Android

Ubaya ni kwamba kuanzia Android Pie kushuka chini huduma hii hawawezi kuipata

  1. Gmail ‘Dark Mode’ Katika iOS
INAYOHUSIANA  Tungulizibomba : Teknolojia mpya ya Kudhibiti Mbu iliyonivutia. #InnovationTZ

Kwa kweli hapa kidogo ni changamoto kwani  iOS  imechuka muda mwingin sana kuhakikisha watumiaji wake wanapta huduma hii ya ‘Dark Mode’ katika App ya Gmail.  Kwa taarifa zilizopo ni kwamba huduma hii itakuja tuu lakini siku na muda kamili imebaki kuwa changamoto

Hivyo basi hatuna budi kusubiria muafaka juu ya jambo hili sio?

Ningependa kusikia kwako, hili umelipokeaje? Niandikie hapo chini katika kisanduku cha maoni. Kumbuka kutembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kila siku kwani daima tupo na wewe katika teknolojia.!

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.