fbpx

apps, TikTok

ByteDance, wamiliki wa TikTok wasema bado watabaki na teknolojia muhimu

bytedance-wamiliki-wa-tiktok-wasema-bado-watabaki-teknolojia

Sambaza

Kampuni ya ByteDance, wamiliki wa app maarufu ya TikTok wamesema bado watabaki na umiliki wa teknolojia muhimu ya app hiyo ata baada ya kukubali kuuza sehemu ya kampuni hiyo nchini Marekani kwa Oracle na Walmart.

Tuliandika kuhusu makubaliano hayo ambayo yanaifanya kampuni ya TikTok kuungana na Oracle na Walmart katika utengenezaji wa kampuni mpya inayokwenda kwa jina la TikTok Global. Katika kampuni hii mpya Oracle na Walmart watamiliki asilimia 20 ya kampuni hiyo.

 

ByteDance, wamiliki wa TikTok wasema algorithm yao itaendelea kuwa siri
ByteDance, wamiliki wa TikTok wasema algorithm yao itaendelea kuwa siri

 

Majukumu ya Oracle:

  • Uhifadhi na usalama wa data za watumiaji wa Marekani na mataifa mengine ukitoa Uchina na
  • Kuangalia kodi-jenga (source code) ya app ya TikTok mara kwa mara kuhakikisha kuna usalama dhidi ya udukuaji

Teknolojia ya algorithm: 

ByteDance wamesema katika makubaliano yao bado ni wao tuu ndio watabaki na siri ya teknolojia kuu ya jinsi aina za post za watumiaji wake zinasambazwa kwenye app hiyo na utumiaji wake.

INAYOHUSIANA  App 5 Bora Za Android Kwa Ajili Ya Kushusha (Download) Muziki!

Teknolojia kuu ambayo watabaki nayo inatambulika kitaalamu kama ‘algorithm’ na ni moja ya teknolojia muhimu zaidi katika mitandao ya kijamii. Inasimamia jinsi gani unaona vitu ambavyo vinatokea pale unapoingia kwenye tovuti husika, kwa kuweza kukuletea posts nzuri basi wanahakikisha unaweza kutumia zaidi tovuti hiyo.

Uamuzi wa kuuza asilimia 20 katika utengenezaji wa kampuni ya TikTok Global umehakikisha kampuni hiyo imeepuka vikwazo kutoka serikali ya Marekani ambavyo vilikuwa vianze mara moja mwanzoni mwa wiki hii.

Je, una mtazamo gani juu ya msimamo wa Marekani wa kutokuwa na imani na makampuni ya Uchina?

Vyanzo: CNBC na vyanzo mbalimbali
Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*