fbpx

Apple, apps, iOS, iOS 14, Teknolojia, Uchambuzi

Unafahamu kuwa iOS 14 imetoka?

unafahamu-kuwa-ios-14-imetoka

Sambaza

Moja ya vitu ambavyo wanaotumia bidhaa za Apple walikuwa wakisubiri ni kutoka kwa iOS 14 ambayo iilitambulishwa Jumatano ya Septemba, 16 2020.

Tunafahamu mwezi Septemba kila mwaka Apple huwa wanatumia kutambulisha vitu mbalimbali ingawa kwa mwaka huu dunia bado inapambana na virusi vya Corona lakini tutegemee kuona vitu vingine vipya kutoka kwa kampuni hiyo nambari moja kwenye masuala ya teknolojia ya simu, bidhaa nyinginezo za kielektroniki. Machache kati ya mengi yaliyomo kkwenye iOs 14 ni:

Muonekano

Toleo hili ni la tofauti na kuvutia kutokana na mpangilio wa programu tumishi, uwezo wa kuweka kwenye kundi moja hivyo kufanya mpangilio wake kuonekana murua.iOS 14

iOS 14

Angalia picha mnato huku ukifanya mengine

Katika miaka ya ya karibuni imeonekana ni vyema kwa kumfanya mtumiaji wa kifaa cha kiganjani kuweza kufanya shughuli mbili kwa wakati mmoja; kwenye iOS 14 Apple wameweka kipengele cha Picha ndani ya Picha (Picture-in-Picture).iOS 14

INAYOHUSIANA  Madhara ya kulala na Simu yako ikiwa Imewashwa

Uwezo wa kuweka jumbe juu kabisa

Kwenye WhatsApp, Telegram inawezekana kabisa kuweka juu kabisa watu ambao unapenda usipate tabu kuwasiliana nao. Sasa hivi ni hivyo hivyo kwenye iOS 14 kwenye iMessage mtu anaweza akachagua ni nani na nani anapenda awaoone juu kabisa akitaka kuona/kusoma jumbe.

iOS 14
Chagua ni jumbe za nani utapenda kuziona za kwanza (mpangilio wa jumbe).

Uwezo wa kubadili kivinjari/uwanja wa kutumia kutumia barua pepe

Kwa yeyote ambaye anatumia iPhone, iPad au hata Apple Watch aanfahamu kuwa kivinjari ambacho kinatumiaka kuperuzi mtandaoni ni Safari lakini pia ukitaka kufikia barua pepe basi itakubidi utumie Mail lakini kwenye iOS 14 unaweza kubadili na kuweka Chrome, Mozilla, Gmail ili kuweza kufika huku na kule kwenye mtandao.

INAYOHUSIANA  Zanzibar kuzima mitambo ya Analogia kwenda Digitali Agosti 31, 2017
iOS 14
Unaweza ukachagua kivinjari gani cha kutumia kwenye iOS 14.

Haya ni kwa uchache tuu lakini mengi zaidi yapo katika mfumo wa picha jongefu lengo likiwa ni kutokukuchosha ewe msomaji wetu.

Vyanzo: MacRumours, The Wall Street Journal

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: ,

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*