fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Samsung simu Teknolojia

Ifahamu simu janja Samsung Galaxy Wide5

Ifahamu simu janja Samsung Galaxy Wide5

Spread the love

Ule msemo wa “Duniani wawili wawili” hata kwenye simu janja pia unaweza kutumika kwani makampuni yanayotengeneza rununu yanaweza kuleta rununu ambazo zinafanana karibu kila kitu.

Samsung Galaxy Wide 5 na Galaxy A22 5G ni mapacha ambao wanafanana karibu kwa kila kitu; naweza kusema kwa zaidi ya 90% sifa za Galaxy Wide 5 ni sawa tuu za kwenye Galaxy A22 5G. Hizi ndio sifa zake:

SOMA PIA  Gallery Go ndio mbadala wa Google Photos

Muonekano|Kipuri mama

Simu hii ina kioo chenye urefu wa inchi 6.6 aina ya LCD huku ung’avu wa kile kinachoonekana kwenye uso wa juu unafikia 1080px+Kwenye upande wa kipuri mama imetumika Dimensity 700 5G.

Kamera|Memori

Kwenye simu hii kuna jumla ya kamera 3 nyuma na moja mbele; ile ya mbele ina MP 48, inayofuatia MP 5 na ya mwisho ni MP 2+taa ya kuongeza mwanga. Kamera ya mbele ina MP 8. Kwenye memori simu hii ina GB 6 za RAM, 128GB diski uhifadhi halikadhalika ina uwezo wa kukubali memori ya ziada ya hadi 1 TB.

Galaxy Wide5

Mpangilio wa kamera za nyuma kwenye Samsung Galaxy Wide 5. Simu hii (Galaxy Wide5) inaweza kufahamika kwa majina mengineyo kama Galaxy Buddy, Falaxy F45 5G,

Uwezo wa betri|Mengineyo

Betri ya kwenye simu hii ni lile ambalo si la kuchomoa na kuchomeka, lina nguvu ya 5000mAh, halikadhalika 15W za teknolojia ya kuchaji haraka. Inatumia USB-C 2.0, Bluetooth 5.1, WiFi 5, teknolojia ya kuweka alama ya kidole imewekwa kwa pembeni, ukubwa wa diski uhifadhi unatofautiana kulingana na nchi ambazo zitauzwa simu hii.

Galaxy Wide5

Muonekano wa mbele na nyuma ambao unajumuisha mpangilio wa kamera.

Mwisho, lakini si kwa umuhimu imezinduliwa huko Korea Kusini kwa ajili ya mtandao wa simu uitwao SK Telecom lakini bei ya Galaxy Wide5 bado hajafamika na inatazamiwa kuingia sokoni hivi karibuni.

Kumbuka kufuatilia TeknoKona ili uweze kuhabarika halikadhalika kuelimika kuhusu teknolojia.

Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania