fbpx

Android, apps, Instagram Lite, Teknolojia

Instagram Lite imerudi na toleo jipya

instagram-lite-imerudi-na-toleo-jipya

Sambaza

Kama ni mtu ambae unatumia simu ya Android na unakuwa makini sana kuhusu suala zima la programu tumishi za kuwa nazo kwenye rununu basi si ajabu ile mitandao ya kijamii mikubwa ukawa unatumia ya toleo la “Lite“.

Tangu mwezi Mei mwaka huu halikuonekana toleo jipya la Instagram Lite lakini Septemba 16 likatoka toleo namba 216. Tangu mwaka 2018, Facebook wamekuwa wakichukulia toleop hili jepesi mahususi kwa majaribio hivyo hata maboresho yake hayatoki mara kwa mara kulinganisha na programu tumishi mama.

Instagram Lite
Instagram Lite toleo jipya.

Kimsingi toleo la Lite ni zuri sana kwa yeyote ambae hapendi kuwa na programu tumishi kubwa kwenye simu janja ilihali rununu ina diski uhifadhi mdogo; Instagram Lite ina ukubwa unaokaribia MB 2 huku ile nyingine ina karibia MB 33.

Pia, kiasi cha intaneti ambacho programu tumishi toleo la Lite linatumia ni kidogo kulinganisha na hizi ambazo ni kubwa ingawa waundaji wamejitahidi kufanya tofauti ya ufanisi kati ya programu tumishi usiwe ni wa tofauti kubwa.

Umaarufu wa Instagram Lite upo Afrika, Kusini mwa Asia na Amerika ya Walatini. Mpaka Mei 2020 ilikuwa ipo katika 20 bora ya programu tumishi zinazosushwa mara kwa mara, nchini Kenya inashikilia namba 8.

Unaweza ukaamua kuishusha kupitia Playstore (kama inapatikana kwenye nchi husika) au ukaipata kupitia APK na kuiweka kwenye simu janja.

Vyanzo: Android Police, Instagram

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*