fbpx
apps, Mtandao wa Kijamii

Kiswahili kuwa lugha ya kwanza Afrika kutambuliwa Twitter

kiswahili-kuwa-lugha-ya-kwanza-afrika-kutambuliwa
Sambaza

Kiswahili hivi karibuni kinatarajiwa kuwa lugha ya kwanza kutoka bara la Afrika kutambuliwa na mtandao wa kijamii, Twitter kwa watumiaji wake kote duniani.

Watumiaji wa Twitter duniani kote wataweza kutafsiri taarifa (tweets) zilizowekwa kwa lugha mbalimbali kwenda kwenye Kiswahili ambacho kinazungumzwa zaidi katika nchi za Afrika Mashariki.

Hili limekuja baada ya jukwaa la kwenye mtandao wa kijamii lililoongozwa na watu wa Afrika Mashariki kutaka Kiswahili kutambulika na kuingizwa katika kutafsiri lugha nyingine.

lugha ya kwanza
Nchi zinazoitumia Kiswahili kama lugha ya taifa au lugha ya kibiashara barani Afrika.

Kufanya ujunbe ufike mbali zaidi, kampeni yenye hashtag #SwahiliIsNotIndonesian na #TwitterRecognizeSwahili imetumika. Kwa muda mrefu machapisho yaliyoandikwa katika lugha ambayo Twitter haiitambui hivyo lugha iliyokuwa inatumika kutafsiri lugha nyingine ni lugha ya Indonesia.

Twitter ilivyokuwa ikivyokuwa haitambui Kiswahili na kufikiri ni lugha ya Indonesia.

Kutambuliwa kwa Kiswahili kwenye Twitter inakuwa ndio lugha pekee mpaka sasa kutoka bara la Afrika. Twitter inatambua lugha 34 mpaka sasa kutoka duniani kote ambapo awali hakukuwa na lugha yoyote kutoka Afrika.

INAYOHUSIANA  Facebook waanzisha uwezo wa kufungua wasifu

Lugha za Afrika zimekuwa zikitambuliwa kama lugha ya Indonesia kitu ambacho kimezua kampeni nyingi mathalani #AfricanLanguagesMatter na #AfricanLanguagesDay.

Kiswahili ni lugha rasmi katika nchi za Tanzania na Kenya na kinazungumzwa sana katika nchi za Rwanda, Burundi, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Msumbiji na Visiwa vya Komoro.

Mipango inaendelea kufanya Kiswahili kuwa lugha rasmi kwa nchi za wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kiswahili kinazidi kufika mbali, tutumie lugha yetu.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.